| Msimamizi wa Mauzo wa Vodacom Tanzania, Bw. Iddy Chitanda (kulia) akimkabidhi wakala wa usajili Bw. Goodluck Clement (kushoto) zawadi ya jiko la gesi na mtungi wake baada ya kujikusanyia pointi nyingi kwa kusajili wateja wapya wengi na wateja hao kununua salio na vifurushi kupitia M-Pesa. Kampuni hiyo inaendesha kampeni ya ‘Loyalty Program’ ikiwa imelenga kuboresha maslahi ya mawakala wake kupitia zawadi mbalimbali kama vile bima ya afya, pikipiki, luninga, simu za mkononi, magodoro, pesa taslimu na ikiwemo safari itakayogharamiwa kila kitu ya kwenda nchini Afrika ya Kusini mwezi Oktoba 2023. |
No comments:
Post a Comment