Foreign Exchange Rates

Equity Bank Advert_12 February 2026

CRDB Bank Advert_070325

Global Sanctions Compliance Masterclass

Friday, 20 March 2026

VODACOM FOUNDATION YAKABIDHI MIUNDOMBINU YA VYOO KWA SHULE MBILI BUTIAMA NA BARIADI

Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa Vodacom Tanzania PLC, Ezekiel Nungwi (wa tatu kushoto), na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Madaraka, Deocray Mtayomba (wa tatu kulia), wakikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua vyoo vipya vya kisasa kumi vilivyojengwa na Vodacom Tanzania Foundation katika Shule ya Msingi Madaraka iliyopo Butiama.
Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa Vodacom Tanzania PLC, Ezekiel Nungwi (kushoto), pamoja na Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Rutherford Magayane (kulia), wakikata utepe kama ishara ya kufungua vyoo vipya vya kisasa kumi katika Shule ya Msingi Sima A iliyopo Bariadi, vilivyojengwa na Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na wadau wake.

Simiyu & Mara, Tanzania – 17 Machi 2026 — Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, kwa kushirikiana na Stanbic Bank Tanzania pamoja na waandaaji wa msafara wa Twende Butiama, imekabidhi rasmi miundombinu ya vyoo katika shule mbili za msingi—Sima A iliyopo Bariadi na Madaraka iliyopo Butiama.

Mradi huo unatekeleza ahadi iliyotolewa wakati wa msafara wa Twende Butiama uliofanyika Julai 2025, uliolenga kumuenzi Julius Kambarage Nyerere na kuhamasisha maendeleo ya jamii, hususan katika sekta za elimu, afya na mazingira.

Kuboresha Mazingira ya Kujifunzia

Kupitia mradi huo, jumla ya matundu 20 ya vyoo vya kisasa—kumi kwa kila shule—yamejengwa, hatua inayolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi pamoja na kulinda afya na ustawi wao.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa Vodacom Tanzania Plc, Ezekiel Nungwi, alisema taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na jamii kuboresha mazingira ya elimu nchini.

Kupitia taasisi yetu tunaamini kuwa uwekezaji katika elimu ni uwekezaji katika mustakabali wa taifa. Ujenzi wa miundombinu hii ni sehemu ya kutimiza ahadi yetu na kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira salama na bora ya kujifunzia,” alisema.

Walimu Wapongeza Mchango

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Sima A, Limi Subi, aliishukuru Vodacom Tanzania Foundation na wadau wake kwa msaada huo, akibainisha kuwa mradi huo utaboresha hali ya usafi na afya ya wanafunzi, na hatimaye kuongeza ufaulu wao darasani.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Madaraka, Deocray Mtayomba, alisema miundombinu hiyo itapunguza changamoto ya uhaba wa vyoo na kuwapa wanafunzi muda zaidi wa kujifunza.

Miundombinu hii itaboresha usafi wa mazingira ya shule na kuwasaidia wanafunzi kutumia muda mwingi zaidi darasani badala ya kusubiri huduma ya choo,” alisema.

Kukuza Afya na Usafi wa Mazingira

Mbali na kuboresha miundombinu ya shule, mradi huo pia unalenga kuhamasisha wanafunzi na jamii kwa ujumla kuzingatia matumizi ya vyoo bora pamoja na kudumisha usafi wa mazingira.

Kupitia miradi yake ya kijamii, Vodacom Tanzania Foundation inaendelea kuwekeza katika sekta muhimu za maendeleo ya jamii—ikiwemo elimu, afya na mazingira—ikiwa na lengo la kuchangia ustawi wa Watanzania na maendeleo endelevu ya taifa.

No comments:

Post a Comment