Foreign Exchange Rates

Equity Bank Advert_12 February 2026

CRDB Bank Advert_070325

Global Sanctions Compliance Masterclass

Saturday, 7 March 2026

MASTERCARD YAITAMBUA EXIM BANK KWA TUZO MBILI ZA ELITE BANKING NA MATUMIZI YA KADI 2025

Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Shani Kinswaga, akipokea moja ya tuzo mbili kutoka kwa Makamu wa Rais Mwandamizi – Meneja wa Nchi, Afrika Mashariki na Visiwa vya Bahari ya Hindi wa Mastercard, Shehryar Ali (wa pili kushoto), wakati wa ziara ya Mastercard katika ofisi za benki hiyo jijini Dar es Salaam. Tukio hilo lilishuhudiwa na Makamu wa Rais na Meneja wa Akaunti wa Mastercard, Elsie Kaguru (kushoto); Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na wa Kati wa Benki ya Exim Tanzania, Andrew Lyimo (wa pili kulia); pamoja na Mkuu wa Uendeshaji na Utoaji wa Huduma wa Benki ya Exim, Tumaini Mwakafwaga (kulia).

Dar es Salaam, Tanzania – Kampuni ya kimataifa ya teknolojia ya malipo, Mastercard, imefanya ziara maalum katika makao makuu ya Exim Bank Tanzania jijini Dar es Salaam, kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimkakati kati ya taasisi hizo mbili pamoja na kukabidhi tuzo mbili muhimu kufuatia mafanikio ya benki hiyo kwa mwaka 2025.

Katika ziara hiyo, Exim Bank Tanzania ilitunukiwa tuzo ya “Best Elite Banking Proposition – 2025” pamoja na “Highest Spend Per Card in Tanzania – 2025”, tuzo zinazoonesha mafanikio yake katika kubuni na kuendesha huduma za kibenki za hadhi ya juu pamoja na kuongoza kwa matumizi ya kadi nchini.

Mafanikio ya Elite Banking

Tuzo hizi zinatokana na mafanikio yaliyopatikana kufuatia uzinduzi wa huduma ya Elite Banking mnamo Julai 2025, huduma iliyobuniwa mahsusi kuwahudumia wateja wa hadhi ya juu (High-Net-Worth Individuals). Huduma hii inalenga kutoa suluhisho za kifedha zinazolingana na mahitaji na mtindo wa maisha wa wateja hao.

Kupitia huduma hiyo, wateja hupatiwa Meneja Mahusiano binafsi (Relationship Manager) anayewasaidia kupata suluhisho za uwekezaji na mikopo ya mtu binafsi. Vilevile, wateja hufaidika na manufaa ya kimataifa ikiwemo upatikanaji wa airport lounges kupitia huduma ya Mastercard DragonPass.

Kuimarika kwa Matumizi ya Kadi

Kwa upande mwingine, tuzo ya “Highest Spend Per Card in Tanzania – 2025” inaonesha mafanikio ya benki katika kuhamasisha matumizi ya kadi kwa wateja wake. Mafanikio hayo yamechangiwa na kampeni mbalimbali za kimkakati, ikiwemo UEFA Priceless Campaign, ambayo ilihamasisha matumizi ya kadi katika malipo huku ikitoa fursa za kipekee kwa washindi kufurahia ofa za kimataifa.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo hizo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Exim Bank Tanzania, Andrew Lyimo, alisema tuzo hizo ni uthibitisho wa mkakati wa benki hiyo wa kuinua viwango vya huduma za kibenki za hadhi ya juu nchini.

Tuzo hizi kutoka Mastercard ni uthibitisho wa mkakati wetu wa kubadilisha na kuinua viwango vya huduma za kibenki za hadhi ya juu nchini Tanzania. Uzinduzi wa Elite Banking mwaka 2025 ulikuwa hatua muhimu katika safari yetu ya kuwahudumia wateja wetu kwa ubora wa hali ya juu, kwa kuunganisha suluhisho bora za kifedha na ofa za kipekee kulingana na mfumo wa maisha ya wateja wetu. Mafanikio haya yanatokana na imani ya wateja wetu pamoja na uwekezaji wetu endelevu katika ubunifu na teknolojia.”

Kwa upande wake, Makamu Rais na Meneja wa Akaunti wa Mastercard, Elsie Kaguru, aliipongeza Exim Bank kwa uongozi wake katika kukuza huduma za premium banking na kuimarisha matumizi ya kadi nchini.

Exim Bank imeonesha uongozi wa kipekee katika kukuza huduma za premium banking na kuimarisha matumizi ya kadi nchini Tanzania. Ukuaji wa haraka wa huduma ya Elite Banking pamoja na kiwango cha juu cha matumizi kwa kila kadi vinaakisi uelewa sahihi wa mahitaji ya wateja wa kisasa. Tunajivunia ushirikiano wetu na Exim Bank na tuna matarajio makubwa ya kuendeleza mafanikio haya kwa pamoja.”

Kuimarisha Malipo ya Kidijitali Tanzania

Ushirikiano kati ya Exim Bank na Mastercard umejikita katika kuimarisha mifumo salama ya malipo ya kidijitali, kuboresha huduma za kadi za hadhi ya juu, na kupanua upatikanaji wa manufaa ya kimataifa kwa wateja wa Tanzania.

Ushirikiano huo tayari umeanza kuonesha matokeo chanya kupitia utofautishaji wa bidhaa za kifedha pamoja na kuongezeka kwa matumizi ya kadi na miamala ya kidijitali.

Ziara hiyo pia imeonesha dhamira ya pamoja ya taasisi hizi mbili katika kukuza malipo ya kidijitali, kuimarisha huduma za kibenki za hadhi ya juu, na kuchochea ukuaji endelevu wa sekta ya fedha nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment