Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Thursday, 15 January 2026

VODACOM YAFUNGUA DUKA JIPYA DODOMA KUKUZA UPATIKANAJI WA HUDUMA KWA WATEJA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Philip Besiimire (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria ufunguzi wa duka jipya la Vodacom jijini Dodoma, linalolenga kusogeza huduma karibu na wateja. Tukio hilo lilishuhudiwa na Mkuu wa Kanda ya Kati, Chiha Nchimbi (wa pili kulia), na Mdau wa Vodacom, Emmanuel Makaki (kushoto).

Dodoma, Tanzania – Vodacom Tanzania PLC imeendelea kuimarisha uwepo wake nchini baada ya kufungua rasmi duka jipya la Vodacom jijini Dodoma, hatua inayolenga kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja wa mji huo na maeneo ya jirani.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. Philip Besiimire, alikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa duka hilo jipya, akisisitiza dhamira ya kampuni kuendelea kuboresha uzoefu wa wateja kupitia huduma bora, za kisasa na zinazopatikana kwa urahisi.

Ufunguzi wa duka hilo ulishuhudiwa na Mkuu wa Kanda ya Kati wa Vodacom, Bw. Chiha Nchimbi, pamoja na Mdau wa Vodacom, Bw. Emmanuel Makaki, ambapo viongozi hao walieleza kuwa uwekezaji huo ni sehemu ya mkakati mpana wa kampuni wa kupanua mtandao wa maduka na kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja katika mikoa mbalimbali nchini.

Duka jipya la Vodacom Dodoma linatarajiwa kutoa huduma mbalimbali ikiwemo usajili wa laini, huduma za kifedha kupitia M-Pesa, mauzo ya vifaa vya mawasiliano, pamoja na huduma kwa wateja binafsi na wa biashara.

Hatua hii inaonesha dhamira ya Vodacom Tanzania katika kuunga mkono maendeleo ya kidijitali, kuchochea uchumi wa ndani, na kuhakikisha wateja wanapata huduma za mawasiliano kwa viwango vya kimataifa.



No comments:

Post a Comment