Dar es Salaam, Septemba 2025 – Kampuni ya teknolojia ya Xiaomi imezindua rasmi simu mpya aina ya Redmi 15C sokoni, ikiwa ni mwendelezo wa jitihada zake za kuwaletea Watanzania suluhisho la kisasa na nafuu katika matumizi ya simu janja.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Erick Mkomoi, alisema simu hiyo imebuniwa mahsusi kukidhi mahitaji ya kila siku ya Watanzania, ikiwa na ubunifu unaoendana na maisha ya kisasa.
Vipengele Muhimu vya Redmi 15C
- Betri ya kudumu zaidi ya saa 24 bila kuchaji tena, huku ikiwa na uwezo wa kuchaji vifaa vingine.
- Kioo kikubwa cha HD kinachomwezesha mtumiaji kutazama maudhui mtandaoni kwa ufasaha.
- Muonekano wa kisasa unaoendana na mazingira ya Kitanzania.
- Teknolojia ya AI inayotambua bidhaa mbalimbali na kumrahisishia mtumiaji kuunganishwa na masoko pamoja na wafanyabiashara.
- Waranti ya miezi 22, ikionesha dhamira ya Xiaomi kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora na uhakika wa ubora wa bidhaa.
Mkomoi alisisitiza kuwa Redmi 15C ni zaidi ya simu ya kawaida, kwani inalenga kusaidia hasa wafanyabiashara wa mtandaoni, kwa kuwawezesha kutumia teknolojia ya AI katika kuongeza fursa za kibiashara na upatikanaji wa masoko.
Kwa uzinduzi huu, Xiaomi inaendelea kuthibitisha nafasi yake kama miongoni mwa makampuni yanayoongoza duniani katika kutoa teknolojia bunifu na zinazowezesha maisha bora zaidi kwa watumiaji wake.

No comments:
Post a Comment