Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Friday, 26 September 2025

LG YAZINDUA DUKA JIPYA LA BIDHAA ZAKE MLIMANI CITY, DAR ES SALAAM

Kutoka kushoto ni Meneja Mkazi wa kampuni ya LG Tanzania, Aashim Wadhwa; Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL, Indrabhuwan Singh; Mkurugenzi wa F&S, Frank Rwamlima; pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji, wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka jipya la LG Electronics lililopo Mlimani City, Dar es Salaam.”

Dar es Salaam, Septemba 24, 2025 – Kampuni ya LG Electronics Kanda ya Afrika Mashariki imezindua duka jipya la bidhaa zake (brandshop) katika Kituo cha Ununuzi cha Mlimani City, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuimarisha uwepo kwenye soko la Afrika Mashariki.

Duka hilo limefunguliwa kwa ushirikiano na kampuni ya F&S pamoja na msambazaji rasmi wa bidhaa za LG nchini, Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL). Hatua hiyo inalenga kuongeza urahisi wa upatikanaji wa bidhaa za LG huku wateja wakipewa huduma za kisasa zenye viwango vya kimataifa.

Kauli Kutoka Kwa Viongozi

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Meneja wa LG Electronics Tanzania, Aashim Wadhwa, alisema:

“Duka hili jipya ni uthibitisho wa dhamira ya LG kuendelea kuwapatia wateja wa Tanzania teknolojia za kisasa na huduma bora zaidi. Dar es Salaam ni jiji lenye kasi kubwa ya ukuaji, na tunaona fursa kubwa ya kushirikiana na ukuaji huo kwa kuwakaribia zaidi wateja wetu na kuhakikisha wanapata msaada wa baada ya mauzo kwa kiwango cha juu.”

Kwa upande wake, mwakilishi wa F&S, Frank Rwamlima, alisema:

“Tunafurahia kushirikiana na LG na MeTL kuwaletea Watanzania uzoefu wa ununuzi wa kisasa. Duka hili litawawezesha wateja kuona na kutumia bidhaa za LG moja kwa moja, na hivyo kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi ya ununuzi katika mazingira ya kiwango cha kimataifa.”

Mwakilishi wa MeTL, Fatema Dewji naye aliongeza:

“Uzinduzi huu ni ishara ya uhusiano unaozidi kukua kati ya MeTL na LG East Africa. LG ni chapa inayotambulika duniani kwa ubora na uimara wake, na duka hili linaonesha dhamira yetu ya pamoja ya kuwaletea Watanzania bidhaa zenye viwango vya juu, imara na za kuaminika.”

Ubunifu na Bidhaa Zitakazopatikana

Katika duka hilo jipya, wateja wataweza kushuhudia na kutumia moja kwa moja ubunifu wa hivi karibuni wa LG, ikiwemo:

  • Vifaa vya nyumbani (home appliances),
  • Vifaa vya burudani majumbani (home entertainment systems),
  • Suluhisho za hali ya hewa (HVAC).

Aidha, kutakuwa na huduma ya haraka, msaada wa baada ya mauzo na uhakika wa kupata bidhaa halisi.

Soko la Afrika Mashariki

Kwa mujibu wa tafiti, soko la vifaa vya nyumbani Afrika Mashariki linatarajiwa kukua kwa wastani wa asilimia 6.55 kila mwaka, huku familia nyingi zikielekeza kipaumbele katika teknolojia endelevu na zinazookoa gharama.

Duka jipya la LG jijini Dar es Salaam ni sehemu ya mkakati mpana wa upanuzi wa kampuni hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki, ambapo tayari imejitanua katika nchi mbalimbali zikiwemo Kenya, Sudan, Ethiopia, Tanzania, Somalia, Uganda, Zambia, Sudan Kusini na Rwanda.

Kupitia uwekezaji huu, LG inalenga kuongeza upatikanaji wa bidhaa zake, kuboresha huduma kwa wateja na kuimarisha uzoefu wa matumizi ya teknolojia za kisasa.










No comments:

Post a Comment