Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Thursday, 29 May 2025

BENKI YA NBC YASHIRIKI MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM, YATOA HUDUMA ZA KIFEDHA KWA WAJUMBE

Mkuu wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya NBC Bw Godwin Semunyu (katikati) sambamba na timu ya wafanyakazi kutoka tawi la benki hiyo jijini Dodoma wakiongozwa na Mkuu wa Kanda ya Kati wa benki ya NBC, Bw Miraji Msuya (wa tano kulia) wakiwa tayari kuwahudumia wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) - Taifa uliofanyika jijini Dodoma, kama sehemu ya juhudi za benki hiyo kutoa huduma za kifedha kwa wateja wake sambamba na kuendelea kujenga mahusiano na wadau wake kibiashara.
Mkuu wa Kanda ya Kati wa benki ya NBC, Bw Miraji Msuya (kulia) akiwaongoza wafanyakazi wengine wa benki hiyo tawi la Dodoma kuwahudumia wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) - Taifa uliofanyika jijini Dodoma.

Dodoma: Mei 29, 2025: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeshiriki kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) - Taifa uliofanyika jijini Dodoma, kama sehemu ya juhudi za benki hiyo kutoa huduma za kifedha kwa wateja wake sambamba na kuendelea kujenga mahusiano na wadau wake kibiashara.

Mkuu wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa NBC Bw. Godwin Semunyu, aliungana na timu ya wafanyakazi kutoka tawi la benki hiyo jijini Dodoma wakiongozwa na Mkuu wa Kanda ya Kati wa benki ya NBC, Bw Miraji Msuya katika ushiriki huo.

Ushiriki wetu kwenye Mkutano huu unatokana na mahusiano yetu kibiashara na wadau wa mkutano huu wakiwemo wanachama mmoja mmoja na chama pia kama taasisi. Pamoja na kufuatilia mkutano huu, NBC kama wageni waalikwa pia tunatoa huduma zetu za kibenki kwa wateja wetu waliohudhuria mkutano hu kupitia timu yetu iliyoweka kambi kwenye eneo hili la mkutano,’’ alisema.

No comments:

Post a Comment