Foreign Exchange Rates

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

Tuesday, 4 February 2025

STANBIC YAENDELEA KUTOA MISAADA KUWEZESHA WATOTO WENYE UHITAJI

Meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Arusha, Hemed Sabuni (kulia) akikabidhi moja kati ya viti 50 kwa mkuu wa shule ya St Jude, Ndaki Saguda (wa pili kushoto), ikiwa ni moja ya jitihada za kurudisha faida kwa jamii kwa kutoa misaada mbalimbali kwa wenye uhitaji katika maeneo tofauti nchini. Benki ya Stanbic imekabidhi viti hivyo ili kuunga mkono juhudi za Shule ya St Jude ya kutoa elimu kwa watoto wenye ufaulu mzuri na vipaji lakini wazazi wao hawana uwezo wa kumudu gharama za elimu. Hafla hii ilifanyika jijini Arusha.
Meneja wa Tawi la Benki ya Stanbic Arusha, Sabuni Hemed (katikati), mkuu wa shule ya The School of St Jude, Ndaki Saguda, (kulia kwake) pamoja na baadhi ya watumishi wa shule hiyo pamoja na Stanbic, wakipiga picha ya pamoja katika hafla ambayo Benki ya Stanbic ilikabidi msaada wa viti 50 kwa shule hiyo.

Benki ya Stanbic Tanzania imetoa msaada wa viti 50 kwa Shule ya St. Jude ya jijini Arusha kuwezesha zaidi ya wanafunzi 1,800 wanaotoka kwenye familia zenye uhitaji kupata elimu.

Msaada huu ambao ni sehemu ya sera ya benki hiyo ya uwajibikaji, katika kurudisha kwa jamii sehemu ya faida yake (CSR), utaimarisha uwezo wa taasisi hiyo katika kutoa elimu bora, kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuwafikia watoto wengi zaidi wenye uhitaji.

Meneja wa Benki ya Stanbic, Tawi la Arusha, Hemed Sabuni aliwakilisha benki hiyo katika hafla ya makabidhiano jijini humo.

No comments:

Post a Comment