Foreign Exchange Rates

Equity Bank Advert_12 February 2026

CRDB Bank Advert_070325

Global Sanctions Compliance Masterclass

Wednesday, 26 February 2025

BENKI YA CRDB YAZIDI KUIPAISHA KILI MARATHON



Hafla ya msimu wa 35 wa mbio za Kili Marathon imefanyika siku chache zilizopita katika viwanja vya ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro, ambapo Benki ya CRDB imeendeleza udhamini wake wa mbio za Kilomita 5 zinazojulikana kama CRDB Bank 5km Fun Run. Kimsingi, huu ni mwaka wa pili mfululizo tangu benki hiyo ianze kufanya udhamini huo, jambo ambalo limezifanya mbio hizo kuendelea kuwa na msisimko mkubwa na wa kipekee.


Akizungumza wakati wa kuhitimisha mbio hizo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko CRDB Bank, Bi. Joseline Kamuhanda amesisitiza kuwa benki ya CRDB inafanya hivyo, kwasababu inatambua na kuthamini umuhimu wa michezo kwa afya na kipato kwa wananchi wakiwemo wateja wao ambao wanawajali sana.

No comments:

Post a Comment