Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, na Diwani wa Kata ya Mwananyama, Bw. Songoro Mnyonge, akikalia moja kiti kilichotolewa msaada katika hafla hiyo. |
Waratibu wa Idara ya Mendeleo ya Manispaa ya Kinondoni wakibeba viti baada kukabidhiwa na Benki ya Biashara DCB jijini leo. |
Akizungumza, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo, Mstahiki meya alisema, hiyo si mara kwanza kwa benki hiyo kuchangia maendeleo katika manispaa hiyo katika sekta za afya na elimu na kusema kuwa misaada hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuhuisha na kuboresha shughuli za maendeleo katika manispaa hiyo.
“Kwa niaba ya Manispaa ya Kinondoni, yaani Mkurugenzi pamoja na madiwani, ningependa kwa dhati kabisa kuishukuru DCB kwa msaada huu utakaosaidia kuweka mazingira bora ya kufanyia kazi kwa watumishi wa Idara hii”.
“Sisi kama manispaa, tunayo furaha kuona benki hii ikirudisha sehemu ya faida yake kwa ajili ya shughuli za maendeleo, ikumbukwe pia hadi kufikia mwaka uliopita, benki imeweza kuleta gawio la zaidi ya shs bilioni 4.3 kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na manispaa zake huku manispaa ya Kinondoni pekee ikipokea gawio zaidi ya shs bilioni 1.3 zinazotumika katika shughuli na miradi ya maendeleo”.
“Hii inatutia moyo sana kuona benki hii inaendelea vizuri, licha ya kuwa zipo benki kubwa zenye ukwasi mwingi lakini bado DCB imekuwa mstari wa mbele katika kurudisha kwa jamii, nitoe rai Kwa benki na Taasisi nyingine kufuata mfano wa Benki ya DCB”.
“Wale ambao hawana akaunti katika benki hii, niwaombe wajiunge na kuweka amana zao katika Benki ya DCB hii ili iweze kujiendesha vizuri na kupata faida na kuendelea kutuhudumia”, alisema mstahiki Meya Mnyonge.
Awali akizungumza mahali hapo, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya DCB, Bw. Emmanuel Barenga aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi katika hafla hiyo alisema msaada huo wameutoa Ili kusaidia juhudi za serikali ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan za kuwaletea wananchi wake maendeleo.
Alisema DCB iliyoanzishwa miaka zaidi ya miaka 22 iliyopita imeendelea kusimamia kwa vitendo maono ya kuanzishwa kwake ambayo yalikuwa ni kuwawezesha wajasiriamali wadogo kiuchumi kwa kuwaletea huduma za mikopo zenye masharti nafuu na fursa nyingine za kimaendeleo.
“Ni Imani yetu msaada huu utakuwa kichocheo kikubwa katika kuboresha huduma katika kitengo hiki, sisi kama DCB hatutaishia hapa tutaendelea kusaidia miradi mingine mbalimbali yenye lengo la kuwakwamua wananchi kiuchumi na kuboresha maisha”, alisema Bw. Barenga.
Naye Bw. Seif Jumanne Seif, Mwenyekiti wa Kikundi cha ujasiriamali cha HASTE, ambao ni Umoja wa wajasiriamali wa wanawake, vijana, wenye ulemavu wanaosaidiwa na Manispaa ya Kionondoni, alitoa shukurani kwa Halmashauri ya Kinondoni pamoja na Benki ya DCB Kwa msaada huo kwani utasaidia utendaji wa kitengo hicho wakiamini kuwa wao kama wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 wataweza kuhudumiwa kwa wakati na kwa ufanisi.
No comments:
Post a Comment