"Tunahitaji kuendelea kuzingatia masuala muhimu kama mabadiliko ya tabianchi na kutathmini athari zake kwenye mazingira ya biashara," aliongeza. Akielezea ushiriki wake hivi karibuni kwenye mkutano wa COP 29, Dkt. Mpango alisisitiza ahadi ya Tanzania katika malengo ya kimataifa ya tabianchi na kusema ni muhimu kujenga uchumi imara licha ya changamoto za tabianchi.
Alisema kuwa kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi kimefikia asilimia 97% kufikia mwaka 2022, upatikanaji wa huduma za afya umeimarika, na kuleta kupungua kwa vifo vya kina mama na watoto wachanga, na uwakilishi wa wanawake katika elimu na nafasi za uongozi umeongezeka.
"Sekta binafsi imekuwa na mchango muhimu katika mafanikio haya, na ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuendelea na juhudi zetu, kuchukua jukumu la uwajibikaji, na kuonyesha uzalendo katika kutekeleza majukumu yetu," alisema. "Pamoja, tunaweza kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050."
Dkt. Mpango alisisitiza ahadi ya Serikali kuimarisha ushirikiano wa umma na sekta binafsi, ambao ni muhimu kwa kukuza maendeleo ya taifa na uchumi.
Katika hotuba yake, Santina Benson, Mkurugenzi Mtendaji wa CEOrt, alisema jukwaa hilo linajivunia hatua mbalimbali za maendeleo ikiwemo kuitisha majukwa za kujadili maendeleo ya kiuchumi, kupitia sekta za viwanda na biashara.
"Miaka hii imekuwa ya mabadiliko makubwa kwa CEO Roundtable, kwani tumepiga hatua kubwa katika maeneo yetu muhimu ya kipaumbele na kuendelea kutumia jukwaa la CEOrt kuanzisha mijadala juu ya masuala muhimu kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi ya nchi," alisema Benson.
Aliongeza kuwa CEOrt imeendelea kufanya juhudi za kukuza uchumi kupitia sekta mbalimbali kama vile nishati, mipango ya urithi wa biashara za familia, maendeleo ya rasilimali watu, fursa za usafirishaji na umuhimu wa uchambuzi wa data katika kukuza maendeleo ya Tanzania.
Katika sherehe hiyo, watu kadhaa mashuhuri walitunukiwa tuzo kwa michango yao ya kipekee kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Tanzania, akiwemo aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrence Mafuru.
Watu mbalimbali, wakiwemo Mabalozi, maofisa waandamizi wa Serikali na wadhamini mbalimbali, wakiwemo CRDB, NMB, Yas, Vodacom, Stanbic Bank, Pepsi, Tiper, KCB Bank, Aris, TCC, TPA, Exim Bank, GSM, Serengeti Breweries, Strategis na Hyatt Kilimanjaro walikuwa ni sehemu ya usiku huo maalum.

No comments:
Post a Comment