Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 25 November 2024

VODACOM NA SANLAM INVEST. WAZINDUA M-WEKEZA, UWEKEZAJI KUPITIA SIMU

Mkurugenzi Mtendaji wa M-Pesa Tanzania, Bw. Epimack Mbeteni, akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya M-Wekeza na Vodacom kwa ushirikiano na Sanlam Investment hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Huduma hii inawawezesha watumiaji kuanza kuwekeza kwa kiasi kidogo cha shilingi 1,000 za Kitanzania wakitumia M-Pesa Super App na kupata faida ya hadi 13% kwa mwaka.
  • Huduma mpya inawawezesha watumiaji kuwekeza wakati wowote na mahali popote
Dar es Salaam, 21 Novemba 2024 – Kampuni inayoongoza katika Teknolojia na Mawasiliano, Vodacom Tanzania Plc kwa kushirikiana na Sanlam Investments East Africa Limited, wamezindua M-Wekeza, huduma ya kibunifu ya uwekezaji iliyoundwa ili kuleta fursa rahisi za uwekezaji kwa watumiaji wa M-Pesa kupitia njia ya kidijitali ya simu zao za mkononi.


M-Wekeza inawawezesha watumiaji kuanza kuwekeza kwa kiasi kidogo cha shilingi 10,000/=, ikitoa faida ya ushindani ya hadi asilimia 13 ya riba kwa mwaka. Huduma hii ya kisasa inaashiria kuingia kwa Vodacom M-Pesa katika masoko ya mitaji, ikileta fursa mpya za ukuaji wa kifedha kwa Watanzania na kuendeleza dhamira ya kampuni hiyo ambayo ni kukuza ushirikishwaji wa kifedha.


Huduma hii inayoletwa kwa kushirikiana na Sanlam Investments East Africa Ltd, mshirika wa uwekezaji aliye na leseni na sifa nzuri, inalenga kurahisisha mchakato wa uwekezaji kwa kila Mtanzania, na kuwawezesha kuongeza kipato chao kwa kuwekeza kwenye vyombo kama dhamana za serikali, masoko ya hisa na masoko mengine ya mitaji salama. Huduma hii inaendana na malengo ya Vodacom ya kukuza ushirikishwaji wa kifedha na kutoa huduma mbalimbali za kifedha kupitia M-Pesa.


Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi wa M-Pesa Epimack Mbeteni alielezea furaha yake kwa kuzinduliwa kwa huduma hii, akisema, "M-Wekeza ni hatua nyingine muhimu katika dhamira yetu ya kuwawezesha Watanzania, kwa kutoa huduma mbalimbali za kifedha kidigitali. Tumebuni huduma hii ili iwe rahisi, ipatikane kwa wote na yenye kuwaletea faida. Iwe wewe ni mwekezaji mzoefu au mpya, M-Wekeza inatoa fursa salama na rahisi ya kuongeza kipato chako kupitia simu yako ya mkononi."


M-Wekeza inadhibitiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Usalama (CMSA), ambayo inahakikisha uwazi na usalama hivyo kuleta imani kubwa katika mchakato wa uwekezaji. Kwa usimamizi imara kutoka CMSA, M-Wekeza inatoa njia salama na ya kuaminika kwa watumiaji wa M-Pesa kushiriki katika masoko ya mitaji yanayokua ya Tanzania.


Mkurugenzi Mtendaji wa CMSA, Nicodemus Mkama, alisisitiza umuhimu wa huduma hii: “Uzinduzi wa M-Wekeza ni hatua ya mabadiliko kuelekea kurahisisha upatikanaji wa fursa za uwekezaji hapa Tanzania. Ushirikiano huu kati ya Vodacom, Sanlam Investments na CMSA unaleta daraja linalowaunganisha Watanzania na masoko ya mitaji na hivyo kuwawezesha watu kutoka tabaka zote za kijamii kuwekeza na kujenga mustakabali wao wa kifedha.”


Jonathan Stichbury, Mkurugenzi Mtendaji wa Sanlam Investments East Africa, pia alizungumzia ushirikiano huu akisema, “Sanlam Investments, tumejidhatiti kukuza ushirikishwaji wa kifedha kupitia suluhisho za kibunifu. Ushirikiano wetu na Vodacom ni hatua muhimu katika kuleta fursa za uwekezaji zinazoweza kufikiwa na zinazovutia kwa Watanzania. M-Wekeza sio tu inatoa riba ya kila siku kwa mapato, bali pia inaruhusu kutoa pesa papo hapo, hivyo kufanya uwekezaji kuwa rahisi na haraka kwa kila mtu.”


Uzinduzi wa M-Wekeza unaimarisha zaidi uongozi wa Vodacom M-Pesa katika sekta ya huduma za kifedha za kidijitali na kuimarisha dhamira ya kampuni ya kuwawezesha Watanzania kwa fursa kubwa za ukuaji wa kifedha, ushirikishwaji na usalama wa fedha zao.

No comments:

Post a Comment