Benki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi, inayokuja na maboresho makubwa kwa wanakikundi wote kufurahia huduma kidijitali.
- Kufungua akaunti kiurahisi na papo hapo kwa kubofya *150*66#
- Kuchangia michango na kukopeshana mikopo ya kikundi kupitia simu zao.
- Kuhamisha fedha kwa wanakikundi bila makato yoyote.
- Kupata taarifa za kikundi kwa uwazi, kwa wakati, na kwa usalama wakati wowote. Taarifa hizi ni kama salio, hela ikitolewa, mwana kikundi akikopeshwa, mtu akiongezwa kwenye kikundi na taarifa nyingine.
- Kujiunga na Bima ya Maisha ya Vikundi ya NMB kwa ajili yao wenyewe na wategemezi wao, kidijitali.
- Kuchangia kupitia chaneli zetu zote, na kupitia mitandao ya simu au kwa kutumia namba maalum ya malipo, yaani Control Number.
Uzinduzi huu umefanyika mbele ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum - Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, na kuhudhuriwa na wanavikundi zaidi ya 400 katika Mtoko na Afisa Mtendaji Mkuu wetu - Bi. Ruth Zaipuna.
Hapa chini ni nukuu za Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna na Waziri Gwajima:
NUKUU CEO NMB
“MABORESHO makubwa yamefanyika yaliyotoakana na mrejesho wa wanachama wa vikundi 200,000 vyenye wanachama zaidi ya Milioni 1 wa iliyokuwa NMB Pamoja Akaunti tuliyoizindua mwaka 2020 hadi kuwa NMB Kikundi Akaunti tunayozindua leo, akaunti ya kidigitali yenye unafuu, urahisi na usalama katika matumizi yake.”
NUKUU DK. GWAJIMA
“PONGEZI ziifikie Menejimenti na wafanyakazi wa Benki ya NMB kwa kuja na NMB Kikundi Akaunti, ambayo ni suluhisho kubwa na mbadala katika utoaji Huduma Jumuishi za Kifedha kwa Vikundi vya Kijamii vya Kuweka Akiba na Kukopa. Huu ni zaidi ya ubunifu katika ustawi na maendeleo ya vikundi na wanachama wake.”
No comments:
Post a Comment