Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 6 December 2023

BRITAM YAADHIMISHA MIAKA 25 UTOAJI WA HUDUMA ZA BIMA

Kutoka kushoto: Tom Gitogo (Group Managing Director wa Britam Holdings PLC), Evelyn Warioba (Director - Britam Insurance Tanzania), Dr. Baghayo Saqware (Commissioner - Tanzania Insurance Regulatory Authority) akimpa zawadi Mike Laiser kumpongeza kwa kua mmoja wa waanzilishi wa Britam Insurance Tanzania miaka 25 iliyopita na Kuria Muchiru (Group Chairman of Britam Holdings PLC).

Kampuni za bima zilianza kuingia rasmi nchini kabla ya Uhuru. Baada ya kutaifisha sekta ya Bima mwaka 1967, ukuaji wa sekta ulififia na ilipofika 1998, Serikali ikaamua kubadili sheria na kukaribisha wawekezaji binafsi katika sekta ya Bima. Kampuni ya Britam ilikuwa ndiyo kampuni binafsi ya kwanza kupewa leseni ya Bima mwaka wa 1998. Baadae kampuni nyingine za Bima zilikuja nchini.


Serikali imeona na inatambua mchango wa kampuni ya Britam Insurance Tanzania Ltd ilivyo msitari wa mbele, na namna kampuni nyingine zote zinavyojitahidi kukuza bima nchini kwa manufaa ya Wananchi na uchumi wa taifa letu.


Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) inajitahidi kujenga uhusiano wa karibu na kampuni binafsi za bima, ili kampuni hizi ziwe na mazingira rafiki ya utoaji huduma kwa Watanzania, hii ni pamoja na kusaidia kutatua majanga yasiyotarajiwa.

Kampuni ya Britam Insurance Tanzania Ltd imekuwa ikitoa huduma za bima zinazowapa wananchi ulinzi wa rasilimali zao, na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ustawi wa uchumi na maisha yetu. Aidha, tunatambua pia mafanikio ya mchango wa kijamii ambao Britam Insurance Tanzania Ltd imekuwa ikiutoa.

Kampuni hii imetoa mchango katika kukuza rasilimali watu kwa ajira zake na mafunzo. Kampuni hii pia inahudumia wateja 47,000 kila mwaka na kulipa kodi serikalini ya takribani shilingi bilioni saba kila mwaka.

Pia Kampuni ina matawi katika mikoa ya Dodoma, Mtwara, Mbeya, Mwanza na Arusha pamoja mawakala nchi nzima.

Kupitia huduma zake katika jamii, kampuni hii imesaidia katika maeneo mengi hasa kwenye miradi ya maendeleo na mpango endelevu wa kuwadhamini na kulipia wanafunzi masomo ya chuo ya bima.

No comments:

Post a Comment