Kama itakavyokumbukwa mnamo tarehe 19 November 2023, Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alimteua Bw. Adam Charles Mihayo kuwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu (CEO) wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB). Bw. Mihayo analeta uzoefu mkubwa katika tasnia ya benki, akiwa amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika nchini Tanzania.
Kufuatia uteuzi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya TCB Dkt. Edmund Mndolwa ameeleza kufurahishwa kwake na uteuzi uliofanywa na Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa Bw. Mihayo Kuwa Mkurugezi Mtendaji wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB PLC). Bwana Mihayo analeta uzoefu na maarifa mapya katika huduma za kisasa za benki hasa wakati huu wa mabadiliko ya kiuchumi unaokua wa nchi yetu. Uongozi wake na utaalam wake utaongeza thamani kwenye benki yetu wakati tunapoendelea kukuza na kupanua huduma zetu ili kuwahudumia wateja wetu vyema zaidi."
Halikadhalika, Dkt. Mndolwa aliongeza kuwa uteuzi wa Bw. Mihayo unaendana na dhima ya Benki ya Tanzania Commercial PLC ambayo ni kutoa bidhaa na huduma kwa urahisi za kibenki kwa kupeleka sokoni bidhaa zenye ubunifu, kuongeza thamani kwa wadau wetu na kuchangia mahitaji ya kijamii na kiuchumi ya nchi.
WASIFU WA BWANA ADAM CHARLES MIHAYO
Bw. Adam Mihayo ana uzoefu wa Zaidi ya miaka 15 katika tasnia ya benki akiwa ameshika nyadhifa mbalimbali za juu katika benki za ndani na nje ya nchi amejiunga na TCB kama Afisa Mtendaji Mkuu baada ya kuteuliwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan tarehe 19 Novemba 2023 akitokea Benki ya Afrika (BOA) Tanzania Limited ambako alikuwa Mkurugenzi Mtendaji.
Kabla ya hapo Bw. Mihayo alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali za juu katika uongozi na masuala ya Benki kama vile Benki ya Absa Tanzania na Benki ya Stanbic Tanzania. Bwana Mihayo Alianza kazi katika Benki ya Biashara (NBC) ambapo alikuwa miongoni mwa vijana wachache waliochaguliwa kupatiwa mafunzo maalum Usimamizi wa masuala ya kibenki katika Benki ya Absa nchini Afrika Kusini mwaka wa 2008.
Bw. Adam Mihayo ni mwananchama wa TBA, Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Kimataifa ya World Savings Bank Institute (WSBI) yenye makao yake makuu mjini Brussels, Mjumbe wa Bodi ya Umoja Switch na Mjumbe wa zamani wa Bodi ya Tanzania Mortgage Refinance Company Limited (TMRC) ambapo pia aliongoza Kamati ya Mikopo ya Bodi.
Bwana Mihayo ana Shahada ya Kwanza ya Biashara (Hons) akichukua fani ya Corporate Finance kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Bw. Mihayo alimshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa heshima kubwa ya kumteua kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) na atafanya kazi bila kuchoka ili kutimiza matarajio ya Rais.

Bw. Mihayo alisema kuwa “Nimefurahi sana kujiunga na TCB kama Mkurugenzi Mtendaji wake mpya. Nitafanya kazi kwa ushirikiano na bodi, menejimenti na wafanyakazi wote katika kuifanya TCB kuwa moja ya wawezeshaji wakuu wa ajenda ya maendeleo ya uchumi nchini”.
KUHUSU TANZANIA COMMERCIAL BANK
Benki ya Biashara Tanzania, iliyokuwa ikiitwa zamani Tanzania Postal bank na baadae TPB Bank Plc, na sasa Tanzania Commercial bank PLC ni benki ya biashara nchini Tanzania na ni moja ya benki kongwe nchini Tanzania, yenye zaidi ya miaka 90, inayotoa huduma mbalimbali za kifedha kwa watu binafsi, wafanyabiashara na taasisi. Benki hii inamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzani kwa zaidi ya asilimia 83%. Baada ya serikali kuunganisha benki zake ya Twiga bankcorp, benki ya Wanawake (Tanzania Women Bank PLC and Benki ya TIB Corporate Limited tarehe 14 Julai 2021 benki ilibadilisha jina na kuwa Tanzania Commercial Bank PLC yenye kaulimbiu ‘Kua Nasi Pamoja’.
Imetolewa na Kitengo cha Uhusiano wa Umma, TCB Makao Makuu
Kazi iendelee
Tanzania Commercial Bank PLC

No comments:
Post a Comment