Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Monday, 2 October 2023
TADB YAWEZESHA DHAMANA YA MIKOPO KWA WAKULIMA
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo (SCGS) imewezesha upatikanaji wa mikopo yenye thamani ya bilioni 221.3 kwa wakulima wadogo nchini.
Akizungumza wakati wa Kongamano la Saba la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Fedha wa TADB Dkt. Kaanael Nnko alisema mikopo hiyo iliyotolewa na Taasisi zakifedha washirika wa TADB kupitia mfuko wa SCGS, umewanufaisha wakulima 16,267
Dkt. Nnko alieleza kuwa zaidi ya asilima 95 ya wanufaika wa mikopo chini ya mfuko huo ni wakulima, wafugaji na wavuvi wadogo pamoja na wajasiliamali wadogo.
Akielezea mikopo hiyo Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa, wanufaika wanawake ni 3,340 ambao wamepatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 16.28 na vijana ni 3,601 waliopatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 13.6.
“Maeneo yaliyofikiwa na Mfuko ni Mikoa 27 sawa na alimia 87 ya Mikoa yote Tanzania Bara na Viziwani na Wilaya 123 sawa na asilimia 83 ya Wilaya zote Tanzania Bara na Visiwani,” alisema
“Mfuko wa SCGS unaosimamiwa na TADB, unasaidia upatikanaji wa dhamana za mikopo ambapo SCGS kwa kushirikiana na taasisi za fedha nchini, inapunguza hatari kwa taasisi hizo ili kuchochea ongezeko la mikopo zaidi kwenye sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambazo ndizo sekta kuu zilizoajiri zaidi ya asilimia 65 ya watanzania wote. Sekta hizi pia zinasaidia upatikanaji wa malighafi za viwandani,” aliongeza
Nnko alisema, Mfuko umechagiza benki kupunguza riba kwa mikopo ya kilimo kwa kuwapatia ukwasi . “Kabla ya kuingia ushirikiano na TADB kupitia mfuko wa SCGS, taasisi za fedha nchini zilikuwa zinatoza riba kati ya asilimia 20 mpaka 36. Lakini, baada ya ushirikiano na kupatiwa ukwasi, benki washirika zimepunguza riba na sasa ni kati ya asilimia 9 mpaka 14 kwa wakulima wadogo. Haya ni mafanikio makubwa ya TADB kupitia mfuko wa SCGS,” alifafanua
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo mpaka sasa TADB kupitia mfuko wa SCGS inashirikiana na taasisi za fedha 16 nchini zenye zaidi ya matawi 700 zikiwemo Benki za Biashara, Benki za Kijamii na Taasisi ndogo za fedha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment