Moja ya faida anayopata mlipaji kupitia NMB Lipa Mkononi ni kuwa wigo mpana wa kulipia kidijitali na kunufaika na rejesho la hadi asilimia 10 katika malipo atakayofanya.
Mhe. Homera aliipongeza NMB kwa ubunifu na kuwaita 'nyumba ya ubunifu’. Aidha, aliishukuru NMB kwa kuzindua kampeni hiyo jijini Mbeya, moja ya mikoa ya mpakani (Zambia na Malawi) ambayo inakabiliwa na matukio mengi ya wizi, ujambazi na upotevu wa pesa, huku akiwataka wafanya biashara na wajasiriamali wa Nyanda za Juu kuchangamkia fursa ya kutumia NMB Lipa Mkononi (QR) ili kukabiliana na changamoto hizo katika mauzo na manunuzi yao ya kila siku.
Vile vile, aliwaasa wana Mbeya - hasa watoa huduma za Bajaji, bodaboda, mama lishe, wauza maduka, wafanyabiashara na wajasiriamali, wanapaswa kuwa vinara katika kuchangamkia huduma hii. Wekeni QR Code hizi madukani na sehemu zenu za biashara, ili kuwawezesha wateja kufanya malipo na kuepukana na mtukio hatarishi kwa fedha zao yanayoikabili jamii, hususani mikoa hio ya mipakani.
No comments:
Post a Comment