Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Tuesday 4 July 2023
BENKI YA NBC YAUNGANA NA TAASISI YA BENJAMIN MKAPA KUTOA UFADHILI WA MASOMO KWA WAKUNGA
Dar es Salaam, Julai 4, 2023: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na Taasisi ya Benjamini Mkapa kuanzia mpango wa kutoa ufadhili wa masomo (scholaships) kwa wanafuzi wa taaluma ya ukunga nchini ili kuunga mkono juhudi za kupambana na changamoto za vifo vinavyotokana na uzazi kwa akina mama.
Kama ilivyo kwa nchi nyingi zinazoendelea, Tanzania inakabiliwa na upungufu wa wafanyakazi wa kutosha kwa ajili ya kuwahudumia wakina mama wajawazito, jambo ambalo hupekea kutokea kwa vifo vingi vinavyoweza kuepukika.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2020, karibu asilimia 95% ya vifo vya akina mama wajawazito vilitokea katika nchi zinazoendelea huku idadi ya vifo hivyo kwa Tanzania ikiwa juu. Pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanyika ikiwa ni pamoja na kuongeza vituo vya afya, kuongeza watumishi wenye ujuzi na nyinginezo.
Ushirikiano kati ya benki ya NBC na Taasisi ya Benjamini Mkapa ni wito wa wadau kuungana katika kulitafutia ufumbuzi tatizo hili. Kupitia ushirikiano huu, NBC itatoa ufadhili wa masomo kwa wakunga na hivyo kuboresha huduma kwa wajawazito lengo likiwa ni kupunguza vifo vinavyoepukika.
Akiongea wakati wa hafla ya utiaji sahihi, Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NBC Theobald Sabi alisema benki ya NBC inayofuraha kutoa mchango wake katika kusaidia kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.
“Tukiwa kama benki inayothamini ustawi wa jamii tunajivunia kutoa mchango wetu kusaidia maendeleo ya jamii ambayo tunaihudumia. Tunafahamu umuhimu na uharaka wa kushughulikia suala la vifo vinavyotokana na uzazi hapa nchini na tunaamini uwekezaji kwenye elimu na mafunzo kwa wakunga wetu kutasaidia sana kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika. Ni furaha kwetu kutoa sehemu ya kiasi kinachopatikana kutokana na uchangishaji fedha wetu wa kila mwaka kupitia mbio za NBC Dodoma Marathon na kuzielekeza kwenye utatuzi wa chagamoto hii,” alisema.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa Dkt. Ellen Mkondya aliishukuru benki ya NBC na kuwataka wadau wengine kufuata mfano wa benki hiyo ili kuongeza nguvu katika kupambana na vifo vinavyotokana na uzazi.
“Tunayofuraha kushirikiana na benki ya NBC katika lengo letu kuu la kupambana na vifo vya wajawazito hapa nchini. Ufadhili wa masomo unaotolewa na benki ya NBC utasaidia kuboresha ujuzi wa wakunga wetu na hivyo kuboresha huduma za uzazi salama,,” alisema.
Kupitia ushirikiano huo wa miaka miwili, NBC itatoa kiasi cha shilingi milioni mia mbili (200m) ambazo zitatumika kusomesha wakunga 100 katika kipindi husika na hivyo kusaidia kuongeza nguvu kazi yenye ujuzi katika kuwahudia akina mama wajawazito.
Benki ya NBC na taasisi ya Benjamini Mkapa zinaamini kuwa uwekezaji katika elimu na mafunzo kwa wakunga ni hatua muhimu sana katika kufikia lengo la Umoja wa Mataifa la Maendeleo endelevu namba 3 ambalo linalenga kusaidia ustawi kwa wote ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.
Kwa maelezo zaidi;
Godwin Semunyu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment