Foreign Exchange Rates

Equity Bank Advert_12 February 2026

CRDB Bank Advert_070325

Global Sanctions Compliance Masterclass

Tuesday, 17 February 2026

NMB YAITANGAZA SEKTA YA MADINI YA TANZANIA KATIKA MINING INDABA 2026, AFRIKA KUSINI

Wajumbe kutoka Benki ya NMB wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde (wa tatu kushoto), pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. James Bwana (wa nne kushoto), wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji katika Mnyororo wa Thamani wa Madini Tanzania lililofanyika jijini Cape Town, Afrika Kusini.
Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, akizungumza wakati wa Kongamano la Uwekezaji katika Mnyororo wa Thamani wa Madini Tanzania, lililoandaliwa na Breakthrough Attorneys kwa ushirikiano na Benki ya NMB.

Benki ya NMB imewakilisha kikamilifu Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya uwekezaji wa madini ya Mining Indaba 2026, yaliyofanyika jijini Cape Town, Afrika Kusini kuanzia Februari 8 hadi 11, 2026.

Kupitia maafisa wake waandamizi, wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Biashara kwa Makampuni, Bw. Nelson Karawa, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo – Idara ya Hazina, Bw. Jeremiah Lyimo, NMB ilitumia jukwaa hilo kuitangaza Tanzania na sekta yake ya madini mbele ya wawekezaji wa kimataifa.

Katika maonesho hayo, NMB ilisisitiza nafasi ya Tanzania kama moja ya nchi zenye rasilimali nyingi za madini na fursa lukuki za uwekezaji barani Afrika, huku ikiweka bayana utayari wa sekta ya fedha nchini kuunga mkono miradi mikubwa ya kimkakati.

Kuonesha Uwezo wa Kifedha na Uzoefu wa Kibenki

Sambamba na ushiriki wake katika mikutano na makongamano ya kimataifa, NMB ilieleza mchango wake katika maendeleo ya sekta ya madini nchini na utayari wake wa kushiriki katika kufadhili miradi mikubwa kupitia suluhisho bunifu za kifedha.

Katika kongamano hilo, Bw. Lyimo alieleza kuwa NMB ina uwezo mkubwa wa kifedha, uzoefu wa kusimamia mikataba mikubwa, pamoja na mtandao mpana wa ndani na nje ya nchi unaowezesha upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya miradi ya madini. Alisisitiza pia nafasi muhimu ya benki katika kuunganisha rasilimali za ndani na kimataifa ili kuharakisha utekelezaji wa miradi mikubwa.

Mkutano wa ‘Investing in Tanzania Mineral Value Chain’

Kwa kushirikiana na Breakthrough Attorneys na Invest Africa, NMB iliandaa mkutano maalum wa wawekezaji uliofahamika kama Investing in Tanzania Mineral Value Chain Conference.

Lengo la mkutano huo lilikuwa kuwatambulisha wawekezaji wa kimataifa fursa zilizopo katika mnyororo mzima wa thamani wa sekta ya madini nchini — kuanzia uchimbaji, uchakataji hadi usafirishaji na masoko — huku ikionesha kuwa mazingira ya biashara Tanzania yameboreshwa na kuwa rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde. Miongoni mwa waliohudhuria ni pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana, pamoja na viongozi kutoka Wizara ya Madini, TISEZA na Tume ya Madini.

Kuimarisha Nafasi ya Tanzania Kimataifa

Ushiriki wa NMB katika Mining Indaba 2026 unaonesha dhamira ya benki hiyo katika kuimarisha nafasi ya Tanzania kwenye ramani ya kimataifa ya uwekezaji wa madini. Pia unaakisi jukumu la sekta ya fedha katika kusaidia utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayochochea ukuaji wa uchumi, ajira na mapato ya taifa.

Kupitia majukwaa ya kimataifa kama haya, NMB inaendelea kuonesha kuwa taasisi za kifedha za Tanzania ziko tayari kushirikiana na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi katika kuendeleza sekta ya madini na mnyororo wake wa thamani kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment