Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 30 May 2023

MKOA WA MARA WAZINDUA RASMI MFUMO WA M-MAMA KURAHISISHA USAFIRI WA DHARURA KWA WAJAWAZITO, WALIOJIFUNGUA NA WATOTO WACHANGA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Mh. Msalika Makungu (wa kwanza kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mratibu wa Kituo cha m-mama katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere eneo la Kwangwa, Bw. Oscar Amos (wa kwanza kushoto) wakati wa uzinduzi wa huduma ya usafiri wa dharura kwa wajawazito, waliojifungua, na watoto wachanga ili kuokoa vifo vya mama na mtoto. Wakisikiliza Pamoja naye wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Dijitali na Huduma za Ziada wa Vodacom Tanzania PLC, Mhandisi Nguvu Kamando na wa pili kushoto ni Mtoa Huduma wa Kituo cha m-mama hospitalini hapo, Bi. Salome Sizya. Mpaka sasa, zaidi ya akina mama 21,800 na Watoto wachanga wamesafirishwa kupitia mfumo huu, ambapo takribani maisha 806 yameokolewa.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Mh. Msalika Makungu (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi wa Dijitali na Huduma za Ziada wa Vodacom Tanzania PLC, Mhandisi Nguvu Kamando (katikati) akielezea namna kampuni hiyo inavyounga mkono juhudi za serikali kuhusu usambazaji wa mfumo wa m-mama unaosaidia kusafirisha akina mama wajawazito, waliojifungua na watoto wachanga kwa dharura ili kuokoa vifo vya mama na mtoto kwa mkoa wa Mara. Akisikiliza kulia wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere eneo la Kwangwa, kushoto ni Mtoa Huduma wa Kituo cha m-mama hospitalini hapo, Bi. Salome Sizya. Mpaka sasa, zaidi ya akina mama 21,800 na Watoto wachanga wamesafirishwa kupitia mfumo huu, ambapo takribani maisha 806 yameokolewa.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Mh. Msalika Makungu (kulia), akikata utepe kuzindua huduma ya usafiri wa dharura kwa wajawazito, waliojifungua, na watoto wachanga ili kuokoa vifo vya mama na mtoto uliofanyika katika Hospitali ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere eneo la Kwangwa, wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Dijitali na Huduma za Ziada wa Vodacom Tanzania PLC, Mhandisi Nguvu Kamando. Mpaka sasa, zaidi ya akina mama 21,800 na Watoto wachanga wamesafirishwa kupitia mfumo huu, ambapo takribani maisha 806 yameokolewa.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Msalika Makungu (kulia), akizungumza na wadau wa sekta ya Afya wakati wa kuzindua huduma ya kuwasafirisha wajawazito, wanawake na watoto wachanga kwa dharura ili kuokoa vifo vya Mama na Mtoto (m-mama), wakati wa hafla iliyofanyika katika Hospitali ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere eneo la Kwangwa, kushoto ni Mkurugenzi wa Dijitali na huduma za Ziada wa Vodacom Tanzania Mhandisi Nguvu Kamando na Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dk Zablon Masatu (katikati). Mpaka sasa, zaidi ya akina mama 21,800 na Watoto wachanga wamesafirishwa kupitia mfumo huu, ambapo takribani maisha 806 yameokolewa.

Wadau wa sekta ya Afya wakipiga makofi kwa Vodacom Tanzania wakati wa uzinduzi wa huduma ya kuwasafirisha wajawazito, wanawake na watoto wachanga kwa dharura ili kuokoa vifo vya Mama na Mtoto (m-mama), wakati wa hafla iliyofanyika katika Hospitali ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere eneo la Kwangwa mkoani Mara. Mpaka sasa, zaidi ya akina mama 21,800 na Watoto wachanga wamesafirishwa kupitia mfumo huu, ambapo takribani maisha 806 yameokolewa.

No comments:

Post a Comment