Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 8 March 2023

WANAWAKE WA SERENGETI BREWERIES WATOA MSAADA WA VIFAA KWA WAJASIRIAMALI WABUNIFU WA TEKNOLOJIA

Mkurugenzi wa masuala ya Sheria na Udhamini wa Wanawake wa Kampuni ya Serengeti Breweries Ltd, Lucia Minde (kushoto), pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiara Wadogo wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Alice Mashiku (wa pili kushoto) wakikabidhi kifaa cha inteneti isiyo na kikomo kwa wanafunzi wanawake wa mambo ya kibunifu ya teknolojia wa kampuni bunifu ya Lauchpad Tanzania wakati wa kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiara Wadogo wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Alice Mashiku (kushoto), akielekeza namna ya kutumia kifaa cha intaneti baada ya kukabidhi msaada wa kifaa hicho kwa kushirikiana na Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa wanafunzi wanawake wa mambo ya kibunifu ya teknolojia wa kampuni bunifu ya Launchpad Tanzania wakati wa kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa masuala ya Sheria na Udhamini wa Wanawake wa Kampuni ya Serengeti Breweries, Lucia Minde.

Dar es Salaam, Jumatano Machi 8, 2023 - Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia mtandao wake wa wanawake ujulikanao kama Spirited Women unaojumuisha wafanyakazi wa kike wa SBL, umetoa vifaa vya intaneti vyenye data bila kikomo kwa mwaka mzima kwa vituo vya ubunifu vya wanawake, katika jitihada za kuchangia kuboresha ushirikishwaji wa wanawake katika sekta ya kidijitali, ambayo inaendana na kaulimbiu ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake (IWD), DigitALL.



SBL’s Spirited Women ilitoa msaada huu kwa kushirikiana na Airtel Tanzania PLC ambapo vituo vinavyolenga wanawake vilipokea ruta za WI-FI, viunganishi vya satelaiti na vifaa vingine vinavyosaidia upatikanaji wa intaneti. Hii ilikuwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake ( IWD ) ya mwaka huu, ambayo inasisitiza ‘Ubunifu na teknolojia ya usawa wa kijinsia’.



Vituo bunifu vya wanawake vilivyonufaika na msaada huu ni LP Digital ya Dar es Salaam, Twende ya Moshi na Ennovate ya Mwanza.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam jana, Meneja Mawasiliano wa SBL na Kiongozi wa Mtandao wa Wanawake wa Spirited woman, Rispa Hatibu alisema, mtandao huo wa Spirited Women kwa kawaida unaunga mkono mipango ambayo itawainua wanawake katika maeneo ya kazi na hata katika ustawi wa kijamii na kiuchumi, hivyo kuunga mkono vituo hivyo vilivyolenga wanawake inaenda sambamba na kile walichodhamiria kufanya.

“Ushirikishwaji ni moja ya nguzo zetu na siku zote tumekuwa tukipenda kutetea makundi ya wanaosahaulika au kutengwa, hivyo tunapoadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake mwaka huu, ilikuwa ni muhimu kwetu kufanya kitu kuwawezesha wanawake katika sekta ya teknolojia kulingana na kaulimbiu ya mwaka huu, na napongeza vituo hivi vya wanawake kwa sababu vinawawezesha wajasiriamali wa kike kukua katika anga ya kidijitali, na hatimaye kuziba pengo kwenye sekta hiyo. Msaada wetu kwa vituo hivi ni kuwapatia huduma ya intaneti ya mwaka mmoja ambayo itawasaidia kupunguza gharama za uendeshaji na kuwawezesha kuwekeza katika kukuza zaidi vituo hivyo,” alisema Hatibu.

Aliongeza kwa kusema kuwa SBL kupitia mtandao wa Spirited Women itaendelea kutoa msaada kwa mipango na miradi inayolenga kuwawezesha wanawake, sio tu kwenye siku ya wanawake duniani (IWD) bali kwa mwaka mzima. Wawakilishi wa SBL’s Spirited Women wa mikoa ya Mwanza na Moshi pamoja na Airtel Tanzania PLC walitembelea vituo vingine viwili vya mikoa hiyo ili kutoa msaada.

Vituo hivyo vitatu vinatoa kozi mbalimbali kuanzia ujuzi wa kufanya masoko kwa njia ya kidijitali pmaoja na kutengeneza mkakati wa biashara. Mbali na programu zinazotolewa, wafanyabiashara wengi wa kike hutembelea vituo hivyo kubadilishana ujuzi na kupata usaidizi wa jinsi ya kuboresha bidhaa zao za kibunifu.

Sambamba na nguzo yake ya ujumuishi, SBL imepiga hatua kubwa kwa kuwekeza katika programu za elimu na mafunzo kwa wanawake vijana, hasa mpango wake wa uanagenzi wa STEM, na programu zake za ufadhili wa kisekta mbalimbali na michango kwa miradi ya kuwawezesha wanawake. Spirited women ni mtandao wa mipango ya uwezeshaji na ushauri ndani ya SBL ambayo inawawezesha wafanyakazi wa kike kukuza taaluma zao hadi nafasi za juu za uongozi.

Kuhusu SBL

Ilianzishwa mwaka 1988 kama Associated Breweries, SBL ni kampuni ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania, na chapa zake za bia zilichukua nafasi ya zaidi ya 25% ya soko kwa ujazo.

SBL ina mitambo mitatu ya uendeshaji Dar es Salaam, Mwanza na Moshi.

Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka wa 2002, biashara hiyo imekuza jalada lake la chapa mwaka hadi mwaka. Upatikanaji wa hisa nyingi na EABL/Diageo mwaka 2010 umeongeza uwekezaji katika viwango vya ubora wa kimataifa na kusababisha nafasi kubwa za kazi kwa watu wa Tanzania.

Kampuni za SBL Brands zimekuwa zikipokea tuzo nyingi za kimataifa na ni pamoja na Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Pilsner Lager, Pilsner King, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness stout na Senator. Kampuni hiyo pia ni nyumbani kwa vinywaji vikali duniani kama vile Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon's Gin, Captain Morgan Rum na Baileys Irish Cream.

No comments:

Post a Comment