Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 9 March 2023

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAWAFIKIA WANAWAKE WENYE UHITAJI HOSPITALI YA OCEAN ROAD CANCER INSTITUTE

Meneja Mawasiliano na Uhusiano Tanzania Commercial bank (TCB), Gloria Mutta (wa tatu kulia) akikabidhi misaada wa vitu mbalimbali kwa Afisa Ustawi wa Jamii wa Hospitali ya Ocean Road Cancer Institute (ORCI), Devotha Kibanga kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wanawake wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam ikiwa ni kusherehekea Siku ya Wanawake inayofanyika kila tarehe 8 ya mwezi wa tatu kila mwaka. Wengine pichani ni wafanyakazi ya hospital.

Katika kusherehekea Siku ya Mwanamke Duniani, Tanzania Commercial Bank (TCB) imeendelea kuwa karibu na wateja wake katika kuzingatia usawa wa kijinsia kwa maisha endelevu.

Tanzania Commercial Bank (TCB) imetumia siku hiyo kuwakumbuka na kuwatembelea wagonjwa wanawake wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Ocean Road na kutoa misaada mbalimbali.


Akizungumza wakati alipotembelea wagonjwa hao Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Benki hiyo, Bi. Gloria Mutta ameeleza kuwa "Tanzania Commercial Bank(TCB) imeendelea kuwa karibu na jamii kwa kutoa misaada mbalimbali hususani kwa wenye mahitaji maalum".

Ameeleza kuwa "Tanzania Commercial Bank (TCB) imetambua mchango wa mwanamke katika kuleta maendeleo".

Aliwahamasisha wanawake hao kuendelea kuiamini na kuitumia Benki hiyo kwani tumekuwa tukitoa misaada mbalimbali pale tunapohitajika.

Bi. Mutta aliongeza kuwa Benki ya TCB inatoa huduma nchi nzima na ina matawi ambayo yanafanya kazi masaa 24 yote hayo ni kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma muda wowote.

Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii Ocean Road Cancer Institute (ORCI), Devotha Kibanga ameishukuru benki hiyo na kusema kuwa imekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada kwa jamii inayotuzunguka hususani sekta ya afya.

No comments:

Post a Comment