Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo, Anna Philemoni ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Benki ya TCB, Diana Myonga. Kushoto ni Meneja wa Tanzania Commercial Bank Tawi la Mlimani City Happy Ernest.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo, Deodarus Nkeyera ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa benki ya TCB, Diana Myonga na kushoto ni Meneja wa Tanzania Commercial Bank Tawi la Mlimani City Happy Ernest.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa benki hiyo.
Tanzania Commercial Bank (TCB) imewahakikishia wateja wake kuwa inabuni mipango madhubuti ya kuzindua bidhaa mpya zinazoendana na mahitaji ya watumiaji wa huduma za kibenki kote nchini.
Akizungumza na wateja wake waalikwa wakati wa wiki ya Huduma kwa Wateja katika Tawi la Tanzania Commercial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB, Sabasaba Moshingi alisema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanatoa huduma bora na yenye kumdhamini mteja.
"Thamani yetu kuu iko katika uhakika kwamba tunamjali na kuvutiwa na mteja, tunataka kuwahakikishia wateja wetu wapendwa kuwa tumejitolea kufanya uzoefu wako wa kibenki kuwa wa kufurahisha zaidi," alisema.
Anna Philemon, mteja wa Tanzania Commercial Bank alisema Benki ya TCB imeweka huduma zake na bidhaa ziko mikononi mwa mteja, na hivyo kuwasaidia wateja kufanya miamala kwa njia rahisi zaidi.
Anna alitoa wito kwa Watanzania kutoka nyanja mbalimbali kujiunga na Tanzania Commercial Bank na kufurahia baadhi ya huduma bora na bidhaa za kipekee zinazotolewa na benki hiyo.
No comments:
Post a Comment