Bank of Africa, inaadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kuwashukuru wateja wake kwa kuendelea kuiamini na kufurahia huduma zake bora mbalimbali. Pia Benki hii ya kimataifa yenye mtandao mkubwa wa shughuli zake barani Afrika, itatumia maadhimisho haya kwa kuwatambua wafanyakazi wake ambao wanaendelea kutoa huduma nzuri kwa wateja katika matawi yake yote nchini.
Maadhimisho haya yenye kauli mbiu ya "Sherehekea Huduma", yataambatana na shughuli mbalimbali katika matawi yote ya Benki nchini kote kama vile kuwazawadia wateja, maswali kuhusiana na utoaji huduma kwa wafanyakazi, Wafanyakazi kuvaa sare maalum, kupamba maeneo ya kutoa huduma pia viongozi wa Benki watapata fursa ya kuwahudumia wateja moja kwa moja kwenye matawi ndani na nje ya kumbi za benki.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho hayo kwenye tawi Kuu la benki lililopo Posta Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Adam Mihayo, alitoa shukrani kwa wateja kwa kuendelea kuiamini Benki kwa miaka mingi. Alisema, "kutoa huduma za kuridhisha wateja na kupata mrejesho na maoni ndio msingi wa shughuli zetu. Tunaamini kwamba siku tunapoacha kutathmini biashara yetu na jinsi huduma yetu inavyoathiri wateja tutakwama kibiashara. Ndio maana, tunaendelea kujitoa kuwapatia huduma bora na kuboresha shughuli zetu."
Maadhimisho ya kila mwaka ya Wiki ya Huduma kwa Wateja hutumiwa kuleta mkazo katika masuala yanayowakabili wateja na kutafuta njia bunifu za kuyashughulikia. Kama benki inayozingatia wateja, BANK OF AFRICA kwa miaka mingi inatumia maadhimisho hayo kuweka mkakati wa kuimarisha huduma bora kwa wateja, kipengele muhimu cha maadili yake ya msingi na pia kupata maoni ya wateja huku ikiwathamini kwa uaminifu wao na uamuzi wa kufanya biashara na Benki.
Kwa kuelewa umuhimu wa ushirikishwaji katika mfumo rasmi wa kifedha na kuonyesha uzoefu wa kutoa huduma bora kwa wateja, benki imefanya uwekezaji ili kuboresha mifumo yake ya kidijitali ikiwa ni pamoja na majukwaa ya huduma za kibenki kwa njia ya simu,mtandao wa interneti, ili kusaidia kujenga jamii isiyotumia pesa taslimu kupata huduma mbalimbali. Huduma za mashine za kutoa pesa (ATM) nazo zimeboreshwa. Benki pia imeanzisha mfumo thabiti unaowezesha wateja wake kufanya miamala ya malipo wakiwa mahali popote.
BANK OF AFRICA – TANZANIA, inajivunia kuwa chini ya mtandao wa Benki mama ya BMCE BANK OF AFRICA, ambayo inafanikisha uendeshaji wa shughuli zake kwa ufanisi. Benki mama, siku zote inaweka mkazo katika dhamira na maono yake ya kuhakikisha inaleta maendeleo kwa wadau wake, inachangia kukuza uchumi sehemu ambapo Benki inafanya kazi, kuboresha huduma kwa wateja na kuwa benki inayopendwa kutumiwa na wateja wengi katika masoko haya. BANK OF AFRICA inatumia mifumo mbalimbali ambayo imefanikisha kuleta ufanisi katika nchi 18.
Ubunifu na huduma kwa wateja ni mambo makuu ambayo BANK OF AFRICA inayazingatia kwa kina. Ili kupata matokeo mazuri katika biashara ya benki, BANK OF AFRICA inaahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja kama ilivyoelezwa katika mkataba wake wa huduma, benki inaahidi: Haki, Usiri, Uaminifu na Uwazi, maadili ambayo yamejengwa na mwongozo wa wafanyakazi wa benki.
No comments:
Post a Comment