Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 4 October 2022

BENKI YA EQUITY IMEZINDUA RASMI WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

 
Bi Leynnette Machibya, (Head of Risk and Compliance) kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Bi Isabela Maganga akihudumia baadhi ya wateja katika uzinguzi wa week ya huduma kwa wateja.

 
Bi Leynnette Machibya, (Head of Risk and Compliance) kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Bi Isabela Maganga akihudumia baadhi ya wateja katika uzinguzi wa week ya huduma kwa wateja.

 

  

Dar es Salaam - Benki ya Equity (T) imezindua rasmi wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar Es Salaam kwenye tawi lake la Mwenge. Wiki ya Huduma kwa Wateja ni wiki ambayo huwa inasherehekewa dunia nzima ikiwa na nia ya kushukuru wateja mbalimbali ambao ndio mchango mkubwa kwa maendeleo ya taasisi. 

Equity Bank inasherehekea wiki hii kwa kauli mbiu ya kipekee ikisema ‘Karibu Memba, Tujienjoy na huduma’. ‘Mteja kwetu ni zaidi ya familia, ni memba. 

Tunahakikisha anapata huduma zote stahiki, kwa wakati na kidijitali’ alisema Bi. Leynette Machibya akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Isabela Maganga. Aliendelea na kusema kuwa Benki yetu imeendelea kuboresha huduma zake na kuhakikisha kuwa inatanua wigo wake wa upatikanaji nchini kama ufunguzi wa tawi letu la Kahama ili kuweza kuwafikia wateja wote Tanzania na kuhakikisha kuwa tunatimiza dhamira yetu ya kubadilisha maisha ya kila Mtanzania.


Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja, Bi. Leynette Machibya aliendelea akisema, huduma zetu ni nafuu zaidi nchini na hivyo kuendana na lengo letu la kukomboa Watanzania kiuchumi kwa kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anatumia mifumo rasmi ya kifedha (financial inclusion). 

Ni benki pekee isiyo na makato yoyote ya mwezi. Tuna huduma mbalimbali ambazo zinamfikia kila Mtanzania, ambazo zikiwemo kutunza akiba, mikopo ya mtu mmoja mmoja, wakulima, wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo, vikundi, waajiriwa, n.k. 

Kuhusu Benki ya Equity Equity Bank (T) ni Benki yenye matawi 15 nchini ikiwa na zaidi ya wafanyakazi 400 ukiwa ni moja ya uwekezaji mkubwa zaidi ulioanzia nchini Kenya na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za Afrika ikiwemo Tanzania, Uganda, Ethiopia, Congo-DRC, Rwanda na Sudan ya Kusini. Kwa maelezo infotz@equitybank.co.tz simu 0768 985 555/ 0768 985 500.   

    

 

No comments:

Post a Comment