Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 4 August 2022

NBC YAENDESHA SEMINA KWA WAFANYABIASHARA JIJINI DODOMA

 Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Mussa Mwinyindaho akiwa katika picha ya Pamoja na wafanyabiashara wa Dodoma mara baada ya Semina ya Wafanyabiashara wa Dodoma iliyofanyika mwishoni wa wiki na kusimammiwa na viongozi waandamizi kutoka Benki ya NBC Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NBC Bwana Mussa Mwinyindaho, akifafanua jambo kwa Wafanyabiashara wa Dodoma (hawapo pichani) kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki ya Biashara mfano, mikopo ya mitaji, mikopo wa ujenzi wa jengo la biashara na bima ya biashara. Aliwaasa wafanyabiashara kwa wakati wote wasisite kufika katika matawi ya NBC kupata huduma za kibenki. 

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), iliandaa chakula cha jioni kilichofanyika katika hoteli ya Morena Dodoma ,ambapo ilialika wamiliki wa Biashara wa mkoa wa Dodoma, kwa lengo la kuongeza ukaribu na wateja wao ambapo benki ya NBC iliwafunda wajasiriamali waliohudhuria hafla hiyo na kuwapa vidokezo juu ya jinsi ya kuboresha biashara zao. 

Benki ya NBC ndiyo Benki kongwe zaidi nchini Tanzania yenye uzoefu wa kutoa huduma kwa zaidi ya miongo mitano, pia inatoa aina mbalimbali za huduma za kifedha kwa wafanyabiashara, zaidi ya hayo, NBC ilishinda tuzo kama taasisi bora zaidi ya kifedha inayosaidia wajasiriamali kwa mwaka 2018, na hivyo kuifanya NBC kuboresha bidhaa na huduma zinazolenga kusaidia wajasiriamali kukuza biashara zao. 

Mkuu wa kitengo cha biashara, benki ya NBC, Mussa Mwinyidaho, aliwashukuru na kuwakaribisha wajasiriamali waliohudhuria hafla hiyo, na kuelezea bidhaa zinazotolewa na benki ya NBC kama vile Mikopo ya kuongeza mtaji unaojumuisha fedha za wasambazaji, dhamana ya utendaji kazi, dhamana ya malipo ya awali, mikopo ya uwekezaji na mikopo ya ujenzi wa majengo ya Biashara. Mbali na hayo benki ya NBC inatoa bima ya biashara ambayo itawasaidia wajasiriamali wakati maafa yanapotokea. 

Mjumbe wa Bodi ya benki ya NBC, Kassim Hussein, alisema NBC ni moja kati ya benki zinazoaminika nchini Tanzania, aliongeza kuwa ni muhimu kwa wajasiriamali kuwa na ujuzi na ufanisi wa kutumia huduma za kibenki, na wawe na uaminifu kwenye kurudisha mikopo na watumiapo huduma nyingine za kibenki, hivyo wajasiriamali wanatakiwa kuwa wabunifu sana, kujitangaza ili waweze kutengeneza wigo mpana wa kupata wateja wengi zaidi na kuongeza kipato kutokana na Biashara zao. 

Bw. Masanga, Mwenyekiti wa Wajasiriamali mkoani Dodoma alisema benki ya NBC ndiyo benki inayotoa huduma bora na msaada kwa wateja wake na kupendekeza kuwa ni muhimu kwa benki hiyo kuanzisha bidhaa nyingine ambazo zitasaidia juhudi za wajasiriamali kwa madhumuni ya kuzalisha mapato na maendeleo ya kiuchumi nchini. Ili kupata maelezo zaidi kuhusu huduma zitolewazo na Benki ya NBC tembelea tawi lolote lililo karibu nawe au tembelea tovuti yao; https://www.nbc.co.tz.

 Wafanyabiashara wa Mkoa wa Dodoma walishukuru Benki ya Taifa ya Biashara kwa kuweza kuwaalika katika hafla hiyo na wamejifunza mengi kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo na kusisitiza ndio benki Bora hapa Tanzania.

No comments:

Post a Comment