Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 31 August 2022

NMB YATANGAZA USHIRIKIANO NA KITUO CHA EFM NA TVE KUFANIKISHA ‘NMB MARATHON 2022’

Kaimu Mkuu wa Habari na Mawasiliano, Vicent Mnyanyika (wa pili kushoto) kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka EFM na TVE, Denis Busulwa (Ssebo), Mratibu wa mbio za NMB Marathon – Suleiman Nyambui na Meneja wa Mbio, David Marealle wakishikina mikono kuonesha ishara ya upendo kwenye kutangaza kituo cha radio cha EFM na TVE kama washiriki wenza.

Benki ya NMB imetangaza ushirikiano na kituo cha Radio cha EFM na TVE kama washiriki wenza katika mbio za NMB Marathon 2022 zinazotarajiwa kufanyika Septemba 24, 2022 katika Viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam, huku kauli mbiu ikiwa "Mwendo wa Upendo".

Mbio hizo zenye lengo la kurudisha tabasamu kwa akina mama wenye matatizo ya fistula kwa kukusanya Sh. milioni 600 ambazo zitaenda kuwasaidia na matibabu katika Hopsitali ya CCBRT.



Akizungumza jana katika uzinduzi huo uliofanyika katika jengo la studio za EFM na TVE, Kaimu Mkuu wa Habari na Mawasiliano kutoka NMB, Vicent Mnyanyika alisema kuwa katika marathon iliyofanyika mwaka jana ambayo ilifanya vizuri hakukuwa na mshirika wa chombo cha habari hivyo msimu huu tumeamua kushirikiana na kituo cha radio cha EFM na TVE katika kukamilisha malengo ya kukusanya Sh. milioni 600.

"Mbio zetu zitakuwa za aina tatu kilometa 5, kilometa 10 na kilometa 21 na gharama zake ni Tsh 20,000 kwa 5km, Tsh 20,000 kwa 10km na Tsh 30,000 kwa 21km.Tukio letu litakuwa kuanzia asubuhi mpaka jioni, baada ya kumaliza mbio, zawadi mbalimbali zitatolewa na kisha tuburudike na wasanii mbalimbali," alisema.



Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka EFM na TVE, Denis Busulwa (Ssebo) alisema furaha ya EFM na TVE kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuinua masuala ya kijamii huku akiamini ushirika wa EFM Na NMB ni ushirika mkubwa unaokutanisha chapa (brand) bora katika kunyanyua masuala ya afya.

Tutakuwa na pre party ya masaa 20 kuelekea siku ya Septemba 24, baada ya hapo washiriki wote waliojisajili watapata nafasi ya kupata supu katika eneo hilo hilo kwa pamoja kisha kuchukuliwa na basi litakalowapeleka mpaka katika viwanja vya Leaders.

Jisajili na NMB Marathon kupitia https://marathon.nmbbank.co.tz/ uwe sehemu ya kurudisha tabasamu kwa akina mama wenye matatizo ya Fistula.

VODACOM YAKABIDHI ZAWADI ZA AWAMU YA SITA PROMOSHENI YA M-PESA IMEITIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mauzo wa kanda ya Dar es salaam na Pwani Vodacom Tanzania PLC, Brigita Shirima (kulia) akimkabidhi funguo mshindi wa Bajaj wa promosheni ya M-Pesa Imeitika kutoka Kimara jijini Dar es Salaam, Magdalena Magoma Moke wakati wa hafla ya kukabidhi Bajaj moja na Bodaboda tano kwa washindi wa awamu ya sita iliyofanyika viwanja vya Barafu Mburahati jijini humo.
Mkuu wa Mauzo wa kanda ya Dar es salaam na Pwani Vodacom Tanzania PLC, Brigita Shirima (wapili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Bodaboda wa promosheni ya awamu ya sita ya M-Pesa Imeitika jijini Dar es salaam.

Kampuni ya teknolojia na mawasiliano ya Vodacom Tanzania Plc, imekabidhi zawadi kadhaa kwa washindi wa awamu ya sita ya M-Pesa Imeitika. Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano hayo, Mkuu wa Mauzo Vodacom kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Brigita Shirima, amesema nina furaha kubwa sana kuwa nanyi leo hapa Viwanja vya Barafu, Mburahati, tunapokabidhi zawadi kwa washindi wetu wa awamu ya sita wa kampeni ya “M-Pesa Imeitika”. 


Kampeni hii ni muendelezo wa juhudi zetu za kuipeleka Tanzania katika Ulimwengu wa kidijitali hususan katika sekta ya kifedha. Kampeni hii ni muendelezo wa juhudi za vodacom za kuipeleka Tanzania katika Ulimwengu wa kidijitali hususani katika sekta ya kifedha. 

Tuesday, 30 August 2022

NMB YAZINDUA ATM YA KUBADILI FEDHA ZA KIGENI KIA

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Hassan Babu akikata utepe kuashiria kuizindua rasmi mashine ya kubadilishia fedha za kigeni kwenda Shilingi za Kitanzania (Forex ATM) ya NMB katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro - Christine Mwakatobe na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Ndg. Juma Irango wakishuhudia.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Hassan Babu akionyesha fedha za kitanzania baada ya kubadili fedha za kigeni kwenye Forex ATM ya NMB iliyozinduliwa rasmi katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro - Christine Mwakatobe.

Benki ya NMB imezindua rasmi mashine ya kubadilisha fedha (Forex – ATM) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) yenye uwezo wa kubadili fedha za kigeni kwenda shilingi za Kitanzania. Hii ni hatua nyingine muhimu kwa Benki ya NMB ya utoaji huduma kwa Watanzania wanaosafiri kutoka nje, watalii na wageni wanaokuja nchini Tanzania.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi uwanjani hapo, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna alisema, wateja na hata wasio wateja wa NMB sasa wanaweza kubadilisha fedha hadi kiasi cha Dola za Kimarekani 2,000 kwa wakati mmoja kwa viwango vya kubadilishia fedha vya Benki ya NMB kwa kujihudumia wenyewe kwa kutumia mashine hii ya ATM katika uwanja huo. Aliongeza kuwa, mashine hii pia inauwezo wa kubadilisha Euro za Umoja wa Ulaya na Pauni ya Uingereza kwenda shilingi ya Tanzania.

Uzinduzi huu ni muendelezo wa huduma hizo zilizozinduliwa kwa mara ya kwanza na NMB Jijini Dar es Salaam kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na Benki hiyo inatarajia kupeleka huduma hizo maeneo mengine ikiwemo uwanja wa ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume (AAKIA) Zanzibar na Zanzibar Stone Town.

NMB BANK INAUGURATES FOREX ATM AT KIA

Kilimanjaro Regional Commissioner, Nurdin Hassan Babu, cuts a ribbon at the Kilimanjaro International Airport over the weekend to launch NMB Bank's foreign exchange ATM. First left is the Bank's CEO, Ruth Zaipuna. Second right is Kilimanjaro Airports Development Company (KADCO) Executive Director, Christine Mwakatobe.

Tanzanians travelling abroad, as well as tourists entering the country can now exchange their money at the NMB Bank Automated Teller Machines (ATMs), thanks to a new service that was launched at Kilimanjaro International Airport (KIA).

“From now on, a customer can exchange up to 2,000 US Dollar at one time at the bank’s exchange rate. This means that a customer can deposit dollars, euros and pounds at the ATM – and get Tanzania shillings, back” said the NMB Bank’s chief executive officer, Ms Ruth Zaipuna. “The service will be accessed by both NMB customers and non-customers.”



Ms Zaipuna said that launch means that cash currency exchange can now be conducted more easily, and faster than before.

“To begin with, this machine will be able to convert USD, Euros and Pounds into Tanzanian shillings,” said Zaipuna.

According to Ms Zaipuna, the presence of the NMB FX ATM machines aims to improve currency exchange services at the airport where the customer will have the opportunity to self-service for 24hrs .

She said that the launch is a continuation of the services launched for the first time by the Bank in Dar es Salaam at Julius Nyerere International Airport (JNIA); the Bank hopes to deliver the service to other places including Abeid Amani Karume International Airport (AAKIA), Zanzibar Airport and Zanzibar Stone Town”.

VODACOM NA DLAB WAHITIMISHA MAFUNZO YA CODE LIKE A GIRL JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi wa Dijitali na Huduma za Ziada Vodacom Tanzania Plc, Nguvu Kamando akizungumza na wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali nchini waliohitimu mafunzo ya Tehama yaitwayo "code like a girl" yanayolenga kuwajengea uwezo katika Tehama na kubuni tovuti, ambayo yameandaliwa na DLab Tanzania na kufadhiliwa na Vodacom Tanzania Plc.
Mwanzilishi Mwenza wa DLab, Mahadia Tunga akizungumza na wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali nchini waliohitimu mafunzo ya Tehama yaitwayo "code like a girl" yanayolenga kuwajengea uwezo katika Tehama na kubuni tovuti, ambayo yameandaliwa na DLab Tanzania na kufadhiliwa na Vodacom Tanzania Plc.




Monday, 29 August 2022

MSIMU WA SOKA LA KIBABE NDANI YA DStv


Malizia mwezi Agosti na mechi za kibabe za #EPL kupitia chaneli za SuperSport ndani ya @dstvtanzania pekee!

Hakikisha unalipia kifurushi chako mapema kwa kupiga *150*53# ufurahie mechi hizi.

#MsimuwaSokalaKibabe

TANZANIA YOUTH ENTREPRENEURSHIP EXPERIENCE BRINGS TANZANIA YOUTH BUSINESS FAIR

Young girls who attended the business fair that showcased different businesses by children in Dar es Salaam.
A group photo of all the children who showcased their businesses at the Children’s business fair organized by Kids Finance with Tracy, Jengahub and Natokajekidijitali.
The Guest of Honour (black coat) Deputy Secretary of the President’s Office – Regional Administration and Local Government visiting the children’s stalls together with Seka Urio, the Regional Manager of NMB Bank (right), Shumabana Walwa, Marketing officer of Multichoice Tanzania and far left Tracy from Kids Finance with Tracy.
Tracy from Kids Finance with Stacy handing over a certificate to John Nelly who was a participant at the Business fair.

Dar es Salaam - 27.08.2022 – Tanzania Youth Entrepreneurship held its 3rd business fair that showcased various businesses launched by young children. The business fair took place at Mtana Restaurant, in Oysterbay, Dar es Salaam on the 27th of August 2022.

Children have dreams and passions, as parents and role models we need to encourage our children to follow their dreams and make a difference in their communities. These kid entrepreneurs teach us how to dig deeply to uncover our passions—and think about how we can use those passions to launch a business. This was an opportunity to show support to these children and their businesses and encourage them.

As we support these young entrepreneurs, we lead the way for a country that creates jobs in the private sector. It also encourages other young children to not give up and they become the faces of the future.

Parents were encouraged to bring their children see their peers showcase their businesses. They were also able to learn more about other businesses, to be encouraged and learn new skills.

NBC WADHAMINI WAKUU - NBC PATRON TROPHY 2022

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa (katikati), akikabidhi vifaa vya mchezo wa Golf kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ), Jenerali Jacob John Mkunda katika mashindano ya "NBC PATRON TROPHY 2022." Pembeni yake kushoto ni Muasisi wa Klabu ya Golf Lugalo, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara na Mwenyekiti TPDF Lugalo Golf - Brig Jen. Mstaafu Michael Luwongo, wa pili Kulia Bw. Elibariki Masuke, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, ambao pia ndio wadhamini wakuu wa shindano hilo. Hafla hii ilifanyika viwanja vya Lugalo Golf Club jijini Dar es salaam hivi karibu.

BENKI YA NBC YADHAMINI KAMPENI YA ‘UZAZI NI MAISHA WOGGING’ KWA UZAZI SALAMA ZANZIBAR


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akianzisha Mbio fupi za kilomita 10 pamoja na matembezi ya kilomita 5 kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar mpaka Uwanja wa Amaan Studium, zilizoandaliwa na Shirika la AMREF HEALTH AFRICA na kudhaminiwa na Benki ya Biashara ya Taifa NBC, ambapo Viongozi mbali mbali wameshiriki katika matembezi hayo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiongoza matembezi ya kilomita 5 yaliyofayika leo kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar hadi uwanja wa Amaan Studium ikiwa ni kampeni ya "Uzazi ni Maisha"yaliyoandaliwa na Shirika la AMREF HEALTH AFRICA na kudhaminiwa na Benki ya NBC, ambapo Viongozi mbali mbali matembezi hayo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiongoza matembezi ya kilomita 5 yaliyofayika leo kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar hadi uwanja wa Amaan Studium ikiwa ni kampeni ya "Uzazi ni Maisha"yaliyoandaliwa na Shirika la AMREF HEALTH AFRICA na kudhaminiwa na Benki ya NBC, ambapo Viongozi mbali mbali matembezi hayo.

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Hussein Mwinyi akimkabidhi cheti cha pongezi Mkurungezi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bw. Theobald Sabi hapo ambapo Benki hiyo walidhamini matembezi ya ya ‘Uzazi ni Maisha Wogging Marathon’ kwa kushirikiana na shirika la AMREF HEALTH AFRICA na Wizara ya Afya ya Zanzibar kampeni ya "Uzazi ni Maisha ambayo imejumuisha wanamichezo mbali mbali kwa matembezi ya kilomita 5 pamoja na mbio fupi za kilomita 10 kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar mpaka Uwanja wa Amaan Studium.

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa MkurungezI Mtendaji wa Benki ya NBC, Bw. Theobald Sabi wakati alipotembelea katika maonesho ya kazi na huduma mbali mbali zinazotolewa na Benki hiyo katika hafla ya Kuchangia Kampeni ya "Uzazi ni Maisha ambayo imejumuisha wanamichezo mbali mbali kwa matembezi ya kilomita 5 pamoja na mbio fupi za kilomita 10 kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar mpaka Uwanja wa Amaan Studium.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkurugenzi Mkaazi wa AMREF HEALTH AFRICA, Dr. Florence Temu katika hafla ya Kuchangia Kampeni ya "Uzazi ni Maisha ambayo imejumuisha wanamichezo mbali mbali ka matembezi ya kilomita 5 pamoja na mbio fupi za kilomita 10 kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar mpaka Uwanja wa Amaan Studium, zilizoandaliwa na Jumuiya ya AMREF HEALTH AFRICA, ambapo Viongozi mbali mbali wameshiriki katika matembezi hayo.
 
Zanzibar, 27 Agosti 2022 – Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Shirika la Amref Health Africa Tanzania, na Wizara ya Afya ya Zanzibar, leo imeendesha kampeni ya ‘Uzazi ni Maisha Wogging Marathon’ katika Uwanja wa Sheikh Amani, Zanzibar, Tanzania. Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Dr. Hussein Ali Mwinyi, alikuwa ndiye Mgeni Rasmi wa tukio hilo la Matembezi, Mbio Fupi na Ndefu (Wogging (Walk-Jog-Run)). 

Kwa kauli mbiu: “Changia Vifaa Tiba kwa Uzazi Salama” matembezi, mbio fupi na ndefu (kwa kifupi ‘wogging’) zilizopata umaarufu zilikazia kutoa elimu kuhusu upungufu uliopo katika sekta ya afya na kukusanya fedha ili kusaidia jitihada za serikali katika kuhakikisha kwamba vifaa tiba na dawa kwa uzazi salama vinapatikana katika vituo vya afya vilivyobainishwa hapa Zanzibar. 

Friday, 26 August 2022

TANZANIA BREWERIES PAYS RECORD 472BN/- IN TAXES


Tanzania Breweries Limited (TBL) is the largest tax payers in form of corporate tax, excise duty and value added tax.

The largest brewer in the land paid 472bn/- last year compared to 463bn/- in the prior year warranting recognition of the largest tax payer in the country.

TBL’s Chairman, Leonard Mususa said during TBL’s 49th Annual General Meeting (AGM) that the tax increase came after the Group revenue grew by 6.0 per cent owing to growth in beer and spirits sales of 5.7 per cent and 3 per cent, respectively.

The firm's operating profit for the period was 179bn/- and profit after tax 134bn/-. Thus dividend per share went up by 60 per cent 255/- for last year. The amount set aside for dividend payment stood at 75bn/-.

The Chairman said they are committed to increasing locally sourced materials as a key partner in the socio-economic development of the country.

“We have committed to ensuring that 100 per cent of the direct farmers in our supply chain are skilled, connected and financially empowered by 2025,” said Mr Mususa.

“Our business will continue to support local farming and sourcing of raw materials”.

NMB BANK, MINISTRY SEAL 100M/- DEAL FOR ‘DIASPORA DIGITAL HUB’

James Bwana (right), Director of Diaspora Department in the Foreign Affairs and East African  Cooperation Ministry and Alfred Shao, NMB Bank Chief of Wholesale Banking responsible for large corporate customers, transactional business as well as Government and International Trade, exchange documents in Dar es Salaam. This was shortly after they signed an agreement between the Ministry and the Bank to finance the development of a Diaspora Digital Hub.

NMB Bank Plc on Thursday pledged 100m/- to Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation for financing the development of the Diaspora Digital Hub that will act as a database for all Tanzanians in the diaspora.

The two parties also signed a Memorandum of Understanding (MOU) to seal the new partnership signed between the Director Diaspora Unit in the Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation Ambassador James Bwana and the NMB Chief Wholesale Banking Alfred Shao.


Mr Shao said after inking he deal in Dares Salaam that the diaspora have a big role to play in the country’s development process adding that the bank will continue investing in systems to enable them accessing stress-free banking products to boost remittance contribution.

“We have already partnered with the government to develop various financial systems now applicable in the market and we are glad working on this new Diaspora Digital Hub,” Mr Shao said.



NMB also has not only established a dedicated department for the diaspora but also come up with a tailor-made system for Tanzanians in the diaspora

Ambassador Bwana said during the event that the government has embarked on a number of strategies to boost the contribution of the Tanzanians in the diaspora to the country’s development.

He said the hub will not only be useful in tracking all the necessary information for Tanzanians in the diaspora but will also be useful in linking them to various services back here in Tanzania like banking and finance services, NIDA services and will be able to know the available investment opportunities back home.



“The Diaspora Digital Hub will help us come up with a national database of all Tanzanians in the diaspora, and it has all the relevant information such as their job descriptions, country of residence. This will help to include them in our development plans,” he said.

According to statistics from the Ministry of Foreign Affairs, Tanzanians in the diaspora remitted 569.3 million US dollars back home last year being a 42 per cent increase in the value of value of diaspora remittances from $400 million in 2020.

BANK OF TANZANIA MONTHLY ECONOMIC REVIEW - JUNE 2022

ECOBANK GROUP LAUNCHES 2022 EDITION OF ITS FINTECH CHALLENGE WITH US$50,000 PRIZE MONEY UP FOR GRABS

  • Fintech Challenge offers early stage and mature start-ups the potential to partner with Ecobank across 33 African countries
  • Applications open until 16 September
Lomé, Togo, 25 August 2022 – Pan-African banking group, Ecobank Group, has launched the fifth edition of the Ecobank Fintech Challenge and encourages African Fintech entrepreneurs to enter the competition.

Fintechs that are aligned with the Bank’s strategic objectives stand a chance to win an overall cash prize of US$50,000 for the top winner and the opportunity to partner and scale their solutions across Ecobank’s 33 African markets.

Fintech companies and developers originating from any of Africa’s 54 countries, as well as global Africa-centered Fintechs, are eligible to enter the Fintech Challenge by visiting: https://Ecobankfintechchallenge.com. Applications can be made until the 16 September 2022.

Ten finalists will be inducted into the Ecobank Fintech Fellowship after the finals and awards ceremony which will take place in October 2022.

USIKOSE ARSENAL VS FULHAM JUMAMOSI HII NDANI YA DStv

 

Arsenal wenye makali sana msimu huu Jumamosi hii watakwenda kuvaana na Fulham ambao wamepanda daraja, Je tutegemee matokeo yapi...?

Lipia mapema kifurushi cha Compact TShs. 51,000/= tu ili usikose burudani hii.

Piga *150*53# kulipia kwa urahisi zaidi @dstvtanzania

#MsimuWaSokaLaKibabe

Thursday, 25 August 2022

VODACOM "BRING YOUR CHILD TO WORK" YAWAJENGEA WATOTO UFAHAMU WA MASOMO YA SAYANSI

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis (kulia) akizungumza na watoto wa wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa masomo ya sayansi na teknolojia (STEM) iliyoambatana na “Bring Your Child to Work" inayoendana na huduma za Vodacom, pia kuwaleta pamoja na kujua wazazi wao wanafanya majukumu gani ya kila siku. Kushoto ni mtoa mafunzo hayo, Dkt. Isaya Ipyana kutoka Taasisi ya Project Inspire.

Kampuni inayoongoza kutoa huduma za teknolojia na mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania imeendelea na mpango wake wa kila mwaka wa kuwezesha watoto wa wafanyakazi wao kuwa na uwezo mzuri wa ufahamu wa masomo ya sayansi na pia kuwaleta pamoja na kujua wazazi wao wanafanya majukumu gani ya kila siku.



Akizungumza kwenye mafunzo hayo Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis alisema " Kupitia mpango huu Vodacom imewaandalia watoto wetu mafunzo ya masomo ya sayansi na teknolojia (STEM) iliyoambatana na “Bring Your Child to Work" inayoendana na huduma za zetu".



Alisema Vodacom ni kampuni ya mawasiliano na teknolojia hivyo wameonelea watoto wakutane pamoja kujua namna gani sayansi na teknolojia inavyofanya kazi ili hapo baadae nao waweze kupenda sekta hii. Mpango huu ni endelevu na ni mwaka wa tano sasa tokea uanzishwe, “Japokuwa tuliusitisha kutokana na janga la uviko 19, na tukawa tunafanya kupitia online.”



Pia mpango huu hauishii tu kuwaleta pamoja watoto bali waliwaandalia program maalum wanapokuwa majumbani ili wasisahau mafunzo waliyopata.


“Vodacom kwenye malengo yetu tunawezesha pia wanafunzi wasichana wa shule za sekondari kote nchini kupitia mpango wa "Code like a girl" ili kuwapa uelewa wa Tehama kwa kubuni tovuti na kupata uwezo wa teknolojia.”

AKIBA COMMERCIAL BANK YAZIDI KUWAFIKIA WATEJA KWA KARIBU ZAIDI

       
Akiba Commercial bank imeendelea kuwafikia wateja kwa karibu zaidi kupitia huduma zake za Wakala zilizosambaa Tanzania nzima. Huduma hii ilizilinduliwa rasmi Agosti, 2021 na sasa Benki inamiliki Wakala 1500 walioko sehemu mbali mbali za Tanzania. 

Huduma hii ya Wakala, imeleta unafuu mkubwa katika upatikanaji wa huduma za kibeki kwa wateja wa ACB, kwani watu wengi zaidi wafikiwa na wanapata huduma kwa haraka na urahisi. Hayo yalisemwa na Mteja wa Akiba, Bw Krantz Mwantepele ambaye ni mteja wa tawi la Ubungo wakati wa mahojiano hayo. Bw. Mwantepele alisema, “ ….. huduma ya Akiba Wakala imenisaidia kupata mahitaji ya kibenki hata baada ya saa za kazi za Benki, kwani inaptikana kwa urahisi mtaani kwangu. Hii inanifanya niweze kufanya miamala kwa urahisi na gharama nafuu. Hakuna ulazima wa kwenda tawini tena. Hakika Akiba Wakala ni zaidi ya huduma kwa kuangalia faida lukuki zilizosheheni katika huduma” 

Naye Bi. Magreth Mwasumbi ambaye ni Meneja Mwandamizi wa huduma za kidijitali kwa Benki ya Akiba, ametoa rai kwa Watanzania wengi kujiunga na Akiba Commercial Bank ili waweze kunufaika na fursa mbali mbali ndani ya Benki hiyo, hususan za kidijitali ambazo zinaleta wepesi, unafuu na uharaka wa upatikana huduma. 

Pia amegusia kuwa Benki inaendelea kuongeza idadi ya mawakala kila siku kufikia mawakala 2,000 mwisho wa mwaka 2022 pamoja na kuboresha na kuanzisha huduma nyingine nyingi za kidijitali kwa ajili ya kuwawezesha wateja kufanya miamala kwa haraka zaidi ndani na nje ya nchi.

JUMAMOSI HII MANCHESTER CITY VS CRYSTAL PALACE


Manchester City wanakwenda kuvaana na Crystal Palace Jumamosi hii ndani ya EPL, Je tutegemee matokeo yapi.

Ni kifurushi cha Compact TShs. 51,000/= tu inayokupa kutazama mechi hii Live tena kwa Lugha Adhimu ya Kiswahili.

Piga *150*53# kulipia kwa urahisi zaidi kifurushi chako.

#MsimuWaSokaLaKibabe

BENKI YA NMB YAPIGA JEKI UIMARISHAJI SEKTA YA UTALII

Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay (kushoto), akikambidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 20 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Pindi Chana (wa pili kushoto), kwa ajili ya ufadhili wa mafunzo kwa wadau wa mnyororo wa thamani kwenye sekta ya utalii. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utalii Tanzania (NCT), Dk. Shogo Mlozi na wa pili kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala.

Benki ya NMB ilikabidhi hundi yenye thamani ya 20m/- kwa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kusaidia kukuza uwezo wa sekta ya utalii hapa nchini.

Msaada huo wa benki hiyo unaunga mkono mkakati wa NCT unaolenga kuongeza ufanisi katika mnyororo wa thamani wa sekta ya utalii kwa lengo la kuboresha huduma wa sekta hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu Rasilimali Watu wa Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay alisema benki hiyo imejipanga kuendelea kusaidia maendeleo ya Sekta ya Utalii na imejidhatiti katika kutoa suluhisho la huduma za kifedha kwa kuwa na mifumo bora zaidi ya ubadilishaji wa fedha na pia kuimarisha biashara ya kadi ambayo itawezesha watalii kutohangaika wanapofanya manunuzi na malipo mbalimbali.

Aidha, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Pindi Chana wakati wa hafla hiyo aliishukuru benki hiyo na kubainisha kuwa Serikali inalenga watalii Milioni tano ifikapo mwaka 2025 hivyo msaada huo umekuja wakati muafaka huku Sekta hiyo inatoa fursa nyingi katika sekta ya benki na fedha.

Wednesday, 24 August 2022

ABSA BANK PARTNERS WITH VISA TO LAUNCH A DEBIT CARD FOR BUSINESSES IN TANZANIA

Absa Bank Tanzania Head of Retail Banking, Ms. Ndabu Lilian Swere (centre), Absa Bank Card Issuing Manager Retail Banking, Elfrida Mruma (right) as well as Absa Bank Head of Marketing and Corporate Relations, Aron Luhanga display the just launched Absa Visa Business Debit Card during a media launch in Dar es Salaam.

Absa Bank Tanzania Limited has partnered with Visa to introduce a debit card targeted at businesses in Tanzania. The Absa Visa Business Debit Card, which is linked to the business’ transaction account, is aimed at helping businesses track and manage operational expenses efficiently, access cost saving benefits and make easy and secure online transactions.

Speaking at the press launch, Ms. Ndabu Swere – Head of Retail Banking, said “At Absa, we are fully committed to delivering innovative solutions that help businesses get things done. This is testament to the numerous “firsts” that Absa has introduced in the market in the last few years, evidenced by the recent recognitions received from Global Brand Magazine where we were awarded as the 2020 Best Digital Bank in Tanzania and 2021 Best Banking Cards in Tanzania.

Therefore, we will continue to bring new disruptive innovations that are going to be a game changer for our clients. We believe that this new Visa business debit card will encourage businesses to shift from cash to digital payments, which is not only the more secure payment option, but also improves efficiency and transparency in the business’ expense management and thus giving businesses better control of their expenditures, and ability to budget and plan for their business growth.”

Tuesday, 23 August 2022

I&M GROUP PLC DELIVERS STRONG GROWTH WITH A 16% INCREASE IN PROFIT AFTER TAX AS IT CONTINUES INVESTMENT IN ITS DIGITAL AND REGIONAL GROWTH STRATEGY

Daniel Ndonye, Chairman, I&M Group PLC speaks at a past event.

Nairobi - I&M Group PLC has sustained its growth momentum into the first half of 2022, with the Group reporting a 16% growth in profit after tax to Kes4.9 billion compared to Kes4.2 billion in the same period in 2021.

During the period under review, the Group’s balance sheet and income improved while strong liquidity and a solid capital base were maintained.

The Group’s total assets grew by 15% to Kes440 billion, up from Kes382 billion in June 2021.

The loan portfolio increased by 13% to Kes231 billion, while investments in government securities were up by 17%.

The net non-performing loans stood at 2.3%, decreasing by 31% year on year on the back of increases in the loan book and recoveries.

Customer deposits closed at Kes.313 billion, a 13% increase year on year.

Net interest income for the period under review recorded a growth of 19%, closing at Kes10.5 billion, an increase from Kes8.9 billion in June 2021, reflecting improved earnings on loans and advances as well as government securities.

The strong growth in non-interest income was driven by a 44% increase in fees and commissions and a jump in foreign exchange trading income from Kes770 million in HY 2021 to Kes1.9 billion.

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YATANGAZA KUPOKEA MAOMBI YA UFADHILI WA MASOMO KWA WANAOSOMEA KILIMO

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Mark Ocitti (katikati) akiongea na waandishi wa habari katika halfa ya uzinduzi wa dirisha la maombi ya programu ya ufadhili wa masomo ya kilimo ya SBL ijulikanayo kama Kilimo Viwanda kwa mwaka 2022/2023. Pembeni yake kushoto ni wanufaika wa program hiyo Winnie Mollel na Hillary Gilbert (kulia) kutoka Chuo cha Kilimo na Mifugo Kaole Wazazi kilichopo Bagamoyo, Mkoani Pwani.

Ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za kuongeza mchanngo wa sekta ya kilimo kwenye uchumi wa nchi, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imetangaza nafasi za ufadhili wa masomo ya kilimo kwa vijana wa Kitanzania wanaotoka kwenye familia zenye kipato duni.

Ufadhili huo unaotolewa kila mwaka, unatolewa chini ya programu ya SBL inayojulikana kama Kilimo Viwanda ambapo wanafuika hulipiwa gharama zote za masomo na kwa kipindi chote wanachokuwa masomoni.

Wanafunzi kutoka Chuo cha Kilimo na Mifugo Kaole Wazazi kilichopo Bagamoyo Mkoani Pwani, Emmanuel Ntandu (wa kwanza kushoto) na Shabani Sabuni, Winnie Mollel, Hillary Gilbert na Clement Abraham Mollel wakishiriki katika ufunguzi wa dirisha jipya la maombi ya programu ya ufadhili wa masomo ya kilimo ya SBL kwa mwaka 2022/2023, ijulikanayo kama Kilimo Viwanda.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa dirisha la maombi kwa mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti alisema programu hiyo imekuwa ikisaidia kuunga mkono jitihada za serikali za kuzalisha wataalamu wapya wa kilimo ambao ni chachu muhimu katika kuwasidia wakulima kuongeza tija katika kilimo chao.

Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), John Wanyancha (kulia) akiongea na waandishi wa habari katika halfa ya uzinduzi wa dirisha la maombi ya programu ufadhili wa masomo ya kilimo ya SBL ijulikanayo kama Kilimo Viwanda kwa mwaka 2022/2023. Kushoto ni Mark Ocitti, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL na Winnie Mollel mnufaika wa programu hiyo kutoka Chuo cha Kilimo na Mifugo Kaole Wazazi kilichopo Bagamoyo Mkoani Pwani.

“Leo hii tunayofuraha kusimama na kusema kuwa programu hii imeweza kuwanufaisha vijana wa kitanzania zaidi ya 200. Baadhi yao wamepata fursa ya kujifunza zaidi kwa vitendo kwenye viwanda vyetu. Lengo letu ni kuona kuwa programu hii inakuwa na matokea chanya kwa sekta ya kilimo na kwa vijana wanaonufaika nayo pia,” alisema

Emmanuel Ntandu ambaye ni mnufaika wa programu hiyo kutoka chuo cha Kilimo na Mifugo Kaole Wazazi kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani na ambaye amepata fursa ya kujifunza kwa vitendo katika kiwanda cha Dar es Salaam alisema “Naishukuru sana kampuni ya SBL kwa kunipatia fursa ya kujifunza zaidi kwa vitendo katika kiwanda chake cha Dar es Salaam kupitia progamu ya Kilimo Viwanda. Nimejifunza mambo mengi na bado naendelea kujifunza.” 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Mark Ocitti (kulia) akiwa na wanufaika wa program ya ufadhili wa masomo ya kilimo ijulikano kama Kilimo Viwanda, Hillary Gilbert (kushoto-mwisho) na Winnie Mollel, wakifungua milango kama ishara ya kuzindua dirisha jipya la mwaka 2022/2023 wa maombi ya ufadhili.

Programu ya Kilimo viwanda ilianzishwa na SBL mwaka 2019 ikilenga kusaidia kuongeza wataalamu wa kilimo kupitia kutoa ufadhili wa masomo. Wanafuika wa programu ni vijana wa Kitanzani wenye ufaulu mzuri darasani na ambao wanatokea katika familia zenye kipato duni.

Katika utekelezaji wa programu hii, SBL imeingia ubai na vyuo vinne vya ndani vinavyofundisha fani ya kilimo ambavyo hupokea wanafunzi wanaolipiwa kupitia programu hii. Vyuo hivyo ni Pamoja na Chuo cha Kilimo na Mifugo Kaole Wazazi kilichopo Bagamoyo Pwani, Chuo cha Kilimo na Mifungo cha Kilacha kilichopo Moshi Kilimanjaro, Chupo cha Kilimo Mt. Maria Goretti kilichopo Iringa na chuo cha Kilomo Igabiro kilichopo Muleba Mkoani Kagera.