Akiba Commercial bank imeendelea kuwafikia wateja kwa karibu zaidi kupitia huduma zake za Wakala zilizosambaa Tanzania nzima. Huduma hii ilizilinduliwa rasmi Agosti, 2021 na sasa Benki inamiliki Wakala 1500 walioko sehemu mbali mbali za Tanzania.
Huduma hii ya Wakala, imeleta unafuu mkubwa katika upatikanaji wa huduma za kibeki kwa wateja wa ACB, kwani watu wengi zaidi wafikiwa na wanapata huduma kwa haraka na urahisi. Hayo yalisemwa na Mteja wa Akiba, Bw Krantz Mwantepele ambaye ni mteja wa tawi la Ubungo wakati wa mahojiano hayo. Bw. Mwantepele alisema, “ ….. huduma ya Akiba Wakala imenisaidia kupata mahitaji ya kibenki hata baada ya saa za kazi za Benki, kwani inaptikana kwa urahisi mtaani kwangu. Hii inanifanya niweze kufanya miamala kwa urahisi na gharama nafuu. Hakuna ulazima wa kwenda tawini tena. Hakika Akiba Wakala ni zaidi ya huduma kwa kuangalia faida lukuki zilizosheheni katika huduma”
Naye Bi. Magreth Mwasumbi ambaye ni Meneja Mwandamizi wa huduma za kidijitali kwa Benki ya Akiba, ametoa rai kwa Watanzania wengi kujiunga na Akiba Commercial Bank ili waweze kunufaika na fursa mbali mbali ndani ya Benki hiyo, hususan za kidijitali ambazo zinaleta wepesi, unafuu na uharaka wa upatikana huduma.
Pia amegusia kuwa Benki inaendelea kuongeza idadi ya mawakala kila siku kufikia mawakala 2,000 mwisho wa mwaka 2022 pamoja na kuboresha na kuanzisha huduma nyingine nyingi za kidijitali kwa ajili ya kuwawezesha wateja kufanya miamala kwa haraka zaidi ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment