Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 29 August 2022

BENKI YA NBC YADHAMINI KAMPENI YA ‘UZAZI NI MAISHA WOGGING’ KWA UZAZI SALAMA ZANZIBAR


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akianzisha Mbio fupi za kilomita 10 pamoja na matembezi ya kilomita 5 kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar mpaka Uwanja wa Amaan Studium, zilizoandaliwa na Shirika la AMREF HEALTH AFRICA na kudhaminiwa na Benki ya Biashara ya Taifa NBC, ambapo Viongozi mbali mbali wameshiriki katika matembezi hayo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiongoza matembezi ya kilomita 5 yaliyofayika leo kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar hadi uwanja wa Amaan Studium ikiwa ni kampeni ya "Uzazi ni Maisha"yaliyoandaliwa na Shirika la AMREF HEALTH AFRICA na kudhaminiwa na Benki ya NBC, ambapo Viongozi mbali mbali matembezi hayo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiongoza matembezi ya kilomita 5 yaliyofayika leo kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar hadi uwanja wa Amaan Studium ikiwa ni kampeni ya "Uzazi ni Maisha"yaliyoandaliwa na Shirika la AMREF HEALTH AFRICA na kudhaminiwa na Benki ya NBC, ambapo Viongozi mbali mbali matembezi hayo.

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Hussein Mwinyi akimkabidhi cheti cha pongezi Mkurungezi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bw. Theobald Sabi hapo ambapo Benki hiyo walidhamini matembezi ya ya ‘Uzazi ni Maisha Wogging Marathon’ kwa kushirikiana na shirika la AMREF HEALTH AFRICA na Wizara ya Afya ya Zanzibar kampeni ya "Uzazi ni Maisha ambayo imejumuisha wanamichezo mbali mbali kwa matembezi ya kilomita 5 pamoja na mbio fupi za kilomita 10 kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar mpaka Uwanja wa Amaan Studium.

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa MkurungezI Mtendaji wa Benki ya NBC, Bw. Theobald Sabi wakati alipotembelea katika maonesho ya kazi na huduma mbali mbali zinazotolewa na Benki hiyo katika hafla ya Kuchangia Kampeni ya "Uzazi ni Maisha ambayo imejumuisha wanamichezo mbali mbali kwa matembezi ya kilomita 5 pamoja na mbio fupi za kilomita 10 kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar mpaka Uwanja wa Amaan Studium.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkurugenzi Mkaazi wa AMREF HEALTH AFRICA, Dr. Florence Temu katika hafla ya Kuchangia Kampeni ya "Uzazi ni Maisha ambayo imejumuisha wanamichezo mbali mbali ka matembezi ya kilomita 5 pamoja na mbio fupi za kilomita 10 kuanzia viwanja wa Maisara Suleiman Jijini Zanzibar mpaka Uwanja wa Amaan Studium, zilizoandaliwa na Jumuiya ya AMREF HEALTH AFRICA, ambapo Viongozi mbali mbali wameshiriki katika matembezi hayo.
 
Zanzibar, 27 Agosti 2022 – Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Shirika la Amref Health Africa Tanzania, na Wizara ya Afya ya Zanzibar, leo imeendesha kampeni ya ‘Uzazi ni Maisha Wogging Marathon’ katika Uwanja wa Sheikh Amani, Zanzibar, Tanzania. Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Dr. Hussein Ali Mwinyi, alikuwa ndiye Mgeni Rasmi wa tukio hilo la Matembezi, Mbio Fupi na Ndefu (Wogging (Walk-Jog-Run)). 

Kwa kauli mbiu: “Changia Vifaa Tiba kwa Uzazi Salama” matembezi, mbio fupi na ndefu (kwa kifupi ‘wogging’) zilizopata umaarufu zilikazia kutoa elimu kuhusu upungufu uliopo katika sekta ya afya na kukusanya fedha ili kusaidia jitihada za serikali katika kuhakikisha kwamba vifaa tiba na dawa kwa uzazi salama vinapatikana katika vituo vya afya vilivyobainishwa hapa Zanzibar. 

Kwa hiyo, tukio hilo lililolenga kuhamasisha taasisi za umma, makampuni na sekta binafsi, watu binafsi pamoja na wadau wengine kuchangia na kutoa msaada wa vifaa tiba na dawa kwa uzazi salama Visiwani. Kampeni hiyo iliwawaleta pamoja zaidi ya washiriki 4,000 ambao ni pamojana maofisa wa ngazi za juu wa makampuni, wanadiplomasia, washirika wa maendeleo, maofisa wa serikali, vyombo vya habari na watu binafsi ambao waliotoa ahadi na kueleza utayari wao wa kusaidia kuchangia kampeni hii kupitia njia mbalimbali za utoaji msaada. Katika kipindi cha miaka mitatu, Kampeni ya Uzazi ni Maisha Wogging inalenga kukusanya zaidi ya Shilingi za Tanzania bilioni moja ikiwemo misaada ya vitu, fedha taslimu na ahadi za kutoa misaada ya vifaa tiba kwa uzazi salama. 

Kampeni itaendeshwa kwa miaka mitatu huku kukiwa na ushiriki wa wadau mbalimbali hadi hapo lengo litakapofikiwa. Mgeni rasmi wa tukio hili, Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, alipongeza juhudi za Amref kwa kubuni njia hiyo ya kipekee na kuwaasa wadau zaidi kushiriki ili kuhakikisha wanakuwa sehemu ya upatikanaji wa vifaa tiba na dawa kwa ajili ya uzazi salama hapa Zanzibar. Alisema michango hiyo mikubwa ni muhimu sana na msaada utakaotolewa utaelekezwa katika kuokoa maisha ya kina mama na watoto wachanga, na hivyo kupunguza vifo wakati wa uzazi, ambavyo vinaweza kuzuiwa hapa nchini. 

“Idadi ya vifo vinavyotokana na matatizo ya uzazi vinavyowaathiri moja kwa moja akina mama na watoto wachanga bado iko juu hapa Zanzibar, ikiwa ni vifo vya akinamama 267 kati ya vizazi hai 100,000 kwa mwaka; na wastani wa vifo 28 vya watoto kati ya vizazi hai 1,000 kwa watoto wachanga (kutokana na takwimu za HMIS 2017). Huduma za mama na mtoto katika vituo vyetu vya afya zina changamoto nyingi ambazo zinachangia katika vifo hivi vitokanavyo na matatizo ya uzazi ikiwemo upungufu wa vifaa tiba, dawa na uhaba wa wahudumu wa afya. Nimetaarifiwa, Kupitia kampeni hii ya Uzazi ni Maisha, jumla ya vituo vya afya 28 vitapata vifaa tiba ambayo ni sawa na asilimia 40.5% ya vituo vyote vinavyotoa huduma ya mama na mtoto katika vijiji vilivyo hapa Zanzibar. 

Namhimiza kila mmoja ajitahidi kuwa sehemu ya mpango huu mwema na kuleta mafaniko kwa Serikali yetu ya Zanzibar,” alisema Mh. Mwinyi. Vile vile, Dkt. Mwinyi aliipongeza Benki ya NBC kwa kushirikiana na Amref Tanzania na kusaidia kampeni hiyo muhimu kwa kushirikiana na serikali ili kupunguza idadi vya vifo vya akina mama hapa Zanzibar. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, akitoa hotuba yake alisisitiza kuwa wana dhamira kubwa ya kuboresha afya ya Mama na Mtoto “Benki ya NBC pia tunaunga mkono ajenda ya taifa ya kuboresha Afya ya mama na mtoto kupitia msaada wa Kliniki za Magari yaani (Mobile Clinic Vans) ambazo tumezitoa kwa serikali kupitia halmashauri za miji ya Unguja-Zanzibar na Dar es Salaam.

 

 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment