Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 1 June 2022

TADB YAENDESHA WARSHA YA UWEZESHAJI JINSIA NA VIJANA KIUCHUMI

Waratibu wa warsha ya TADB Uwezeshaji Jinsia na Vijana Kiuchumi iliyofanyika mkoani Dar es Salaam. Kutoka kushoto walioketi ni Mihaela Marcu, Meneja wa Programu wa masuala ya vyombo vya kifedha kutoka Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Mzee Kilele, Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa TADB, Sarah Weiss Mshauri wa mifumo ya Kimaendeleo ya Kifedha kutoka ICR na Emmanuely Lyimo, Meneja Uhamasishaji wa Rasilimali kutoka TADB.

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeandaa mpango mkakati wa kuwawezesha kiuchumi wanawake na vijana kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji kijulikanacho kama Investment Climate Reform Facility (ICR).

Mkakati huu umeanza na warsha ya mashauriano baina ya TADB na ICR ili kujadili juu ya mpango wa kuwainua kupitia misaada mingine muhimu inayohitajika ili kuwainua kiuchumi wanawake na vijana kwenye kilimo.

Juhudi za TADB zinalenga kwa makusudi katika kuziba pengo la kiuchumi kati ya wanawake na vijana, kwani takwimu za Finscope zinaonyesha kuwa asilimia 50 ya nguvu kazi lakini hawajajumuishwa katika sekta rasmi ya fedha, na asilimia 6 tu ya wanawake hawana akaunti za benki huku benki na asilimia 26 pekee ya vijana wakiwa wakulima.

TADB imeanzisha warsha hii ili kupata utaalamu zaidi wa kiufundi kutoka kwa Kituo cha ICR kinachofadhiliwa na Umoja wa Ulaya ambapo mpango huu unalenga kuifahamisha TADB na taasisi nyingine za fedha kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuongeza ushirikishwaji wa kifedha miongoni mwa wanawake na vijana katika sekta ya kilimo.

Washiriki wa warsha hiyo ya siku mbili ya mashauriano ni pamoja na wawakilishi kutoka wizara mbalimbali za serikali ya Tanzania bara na Zanzibar, Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, mashirika ya wanawake na vijana, na wawezeshaji wa soko. Washiriki walipata fursa ya kujadili maoni yao kuhusu bidhaa na huduma za kilimo kwa wanawake na vijana.

Warsha hiyo ilihitimisha kuwa mpango wa uwezeshaji unapaswa kujumuisha aina mbalimbali za bidhaa za kifedha kama vile utaratibu wa udhamini, utoaji wa mikopo ya moja kwa moja, na njia za mikopo kwa taasisi za fedha washirika. Mpango huo pia utajumuisha ushirikiano kati ya TADB na wawezeshaji wa soko ili kutoa taarifa za soko, mafunzo, na kukuza uwezo kwa wakulima wachanga na wanawake.

About TADB:

Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) is a state-owned development finance institution (DFI) established to catalyse development of the agriculture sector in Tanzania. TADB mission is to facilitate development and support transformation of the agriculture sector by providing short, medium and long term finance to agriculture projects in Tanzania that promotes economic growth, food security and reduction of income poverty.

About ICRF:

The ICR Facility is co-funded by the European Union (EU), the Organization of African, Caribbean and Pacific States (OACPS) under the 11th European Development Fund (EDF), together with the German Federal Ministry for Economic Cooperation and Development (BMZ) and the British Council. It is implemented by Deutsche Gesellschaft für Internationale Zusammenarbeit GmbH (GIZ), the British Council (BC), Expertise France (EF), and Stichting Nederlandse Ontwikkelingsorganisatie (Netherlands Development Organization, SNV).

For more info, please contact:

Theresia Christian
Senior Public Relations & Marketing Officer
4th Floor Acacia Estate,
Tel: +255 743 057 318
Email: theresia.christian@tadb.co.tz

No comments:

Post a Comment