Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 9 May 2022

BANDARI YA DSM KUWEKA REKODI NYINGINE JUMATATU HII


*Meli kubwa ya MERIDIAN ACE

Meli kubwa ya shehena ya magari inatarajia kuwasili kwenye bandari ya Dar es Salaam. Meli hiyo kutoka Japan na Singapore itawasili Dar es Salaam Mei 9, 2022 ikiwa na magari 4,397 idadi ambayo haijawahi kufikiwa kwa pamoja. Hii ndio rekodi kubwa kuliko zote. Rekodi ya mwisho ilikuwa magari 4,041 yaliyowasili Aprili 08 2022.



Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA Bw. Nicodemus Mushi imesema, mafanikio hayo ni matokeo ya kazi kubwa ya kutangaza Uwezo wa Bandari za Tanzania, inayofanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Awamu ya Sita kote ulimwenguni.



Amesema uwekezaji mkubwa umefanywa na Serikali katika Vitendea kazi na Maboresho ya Miundombinu ya kibandari sambamba na Kampeni za Kimasoko na ushirikiano thabiti wa TPA, wateja na wadau wake wengine.

No comments:

Post a Comment