Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 25 January 2022

WAZIRI WA HABARI ATEMBELEA OFISI ZA VODACOM

  • Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye atembelea ofisi za Vodacom na kusisitiza ushirikiano
  • Aipongeza Vodacom kwa kukuza uchumi wa nchi

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza kwenye mkutano na Watendaji Wakuu wa Kampuni ya Mawasiliano Vodacom pamoja na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kutembelea makampuni ya simu akiambatana na viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni hiyo, Jaji mstaafu Thomas Mihayo, Mkurugenzi Mkuu Vodacom , Sitholizwe Mdlalose na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano, Rosalynn Mworia.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (katikati) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Bodi,  Kampuni ya Vodacom Jaji mstaafu Thomas Mihayo (wa pili kushoto), Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Vodacom, Margaret Ikongo (wa pili kulia) Mkurugenzi Mkuu Vodacom Tanzania, Sitholizwe Mdlalose (kulia) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano, Rosalynn Mworia (kushoto), wakati wa ziara yake ya kutembelea makampuni ya simu hivi karibuni.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Sitholizwe Mdlalose. Anayeshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia mara baada ya ziara ya Waziri huyo kwenye Makao Makuu ya ofisi za Vodacom jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha Vodacom Tanzania, Hilda Bujiku akielezea mbele ya Waziri na Watendaji wa Vodacom na TCRA namna ambavyo mpango mkakati wa fedha wa mwaka 2021-22 unavyofanya kazi.
Meneja wa Maduka ya Rejareja Vodacom, Vanessa Mlawi (kulia) akielezea ubora wa bidhaa na huduma zinazotolewa kwenye maduka ya Vodacom yaliyotapakaa nchi nzima kwa Waziri wa Habari, Nape Nnauye alipotembelea Makao Makuu ya Kampuni hiyo hivi karibuni.



No comments:

Post a Comment