| Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Pamela Nchimbi (wa pili kulia) akitoa elimu ya masuala ya maendeleo endelevu katika kongamano la wanawake lililoandaliwa na Kampuni ya ushauri wa masuala ya kifedha ya Bridge Consult kwa udhamini mkuu wa Benki ya DCB jijini Dar es Salaam. Lengo la jukwaa hilo ni kubadilishana mawazo na kupeana ujuzi wa masuala ya kifedha, uwekezaji pamoja na maendeleo endelevu. Kutoka kulia ni Mtaalamu wa masuala ya Kimaisha, Mihaela Marcu, Mshauri wa masuala ya afya kwa jamii, Naomi Serbantez na Mkurugenzi wa Mgahawa wa Terrace, Sarah Raqey. |
No comments:
Post a Comment