Meneja Uvumbuzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Bertha Vedastus akiongea na wateja wa kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa bia ya Guinness Smooth uliofanyika jijini Mbeya hivi karibuni . |
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, wakisakata sebene muda mfupi baada ya uzinduzi wa bia ya Guinness Smooth uliofanyika jijini Mbeya. |
Baadhi ya wateja wa Kampuni ya Bia ya Serengeti wakifurahia bia ya Guinness Smooth wakati wa uzinduzi wa bia hiyo kwa Kanda za Nyanda za Juu Kusini uliofanyika jijini Mbeya. |
Guinness smooth ni bia mpya ndani ya familia ya kubwa na kongwe duniani ya Guinness. Bia hii ina ladha murua ambayo huwafanya watumiaji wake kuifurahia kila mara wanapoitumia ikiwa na sifa zilizoongezwa vionjo za bia ya Guinness.
Akiongea wakatii wa uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika jijini Mbeya, meneja uvumbuzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti ambao ndiyo watengenezaji wa bia hiyo alisema uzinduzi huo wa kanda zanyanda za juu kusini unafanyika baada ya uzinduzi uliokuwa na mafanikio wa Dar es Salaam na kanda ya kaskazini.
“Wakazi wa kanda ya Nyanda za juu kusini wamekuwa ni waaminifu kwa bidhaa za SBL na kwa namna ya pekee tuwashukuru kwa kuchagu bidhaa zetu. Ikiwa kama sehemu ya kuwaonyesha mapenzi yetu kwao, leo tunawaletea bia mpya ya kimataifa ambayo itawapa uzoefu wa kipekee kila wanapoitumia,” alisema
Meneja uvumbuzi huyo alisema alisema bia ya Guinness Smooth imtengenezwa kwa kumjali mtumiaji bia wa Kitanzania ikiwa la ladha ya kipekee na kuongeza kuwa bia hiyo inatengenezwa kwa kiasi kikubwa cha malighafi za ndani kwenye kiwanda cha SBL kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro
Bertha alisema bia mpya ya Guinness Smooth inathibitisha nia ya kampuni ya bia ya Serengeti kuwapatia bidhaa bora zenye viwango vya kimataifa lakini katika bei ambayo kila mtu awaeza kuimudu.
No comments:
Post a Comment