Wachezaji wa timu ya kikapu Mkoa wa Dar es Salaam wakifurahi baada ya timu hiyo kuibuka washindi wa Kitaifa wa mashindano ya CRDB Taifa Cup 2021 yaliyofanyika Jijini Dodoma kwa kuwashinda timu ya Mkoa wa Arusha katika fainali.Timu ya mpira wa kikapu Mkoa wa Dar es Salaam wanawake wakifurahia ushindi wao baada ya kukabidhiwa kombe na mfano wa hundi ya shilingi milioni sita na laki tano kwa kuibuka washindi wa mashindano ya CRDB Taifa Cup 2021 yaliyofikia kilele chake mwisho wa wiki Jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi (katikati) akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya mpira wa kikapu Mkoa wa Dar es Salaam, Omari Juma (kulia) mara baada ya timu hiyo kuibuka washindi wa Kitaifa wa CRDB Taifa Cup 2021 yaliyofanyika Jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurungenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi (katikati) akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya mpira wa kikapu wanawake Mkoa wa Dar es Salaam, Hadija Kalambo (kulia) mara baada ya timu hiyo kuibuka washindi wa Kitaifa wa CRDB Taifa Cup 2021 yaliyofanyika Jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurungenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.

Mfungaji bora wa kiume kutoka Timu ya kikapu ya Mkoa wa Arusha, Tyrone Edward akikabidhiwa kombe lake.
Mashabiki wakifuatilia Michezo ya fainali.
Timu ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (jezi Nyeusi) wakichuana na wenzao wa Arusha. Timu ya Dar es Salaam ilishinda kwa 71-52.
Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam (Blue Bahati) wakichuana na Timu ya Kikapu Unguja. Timu ya Dar es Salaam ilishinda kwa 67 - 55.
Na Mwandishi wetu,Dodoma.

Timu za mpira wa kikapu za kiume na wanawake za mkoa wa Dar es Salaam zimefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya CRDB Benki Taifa Cup kwa mwaka huu.
Wakati timu ya wanawake ya Dar es Salaam ikitwaa taji hilo kwa kuifunga Unguja kwa pointi 67-55, Timu ya wanaume ilifanikiwa kutwaa taji hilo kwa kuwachabanga Arusha kwa pointi 71-52. Michezo hiyo ilifanyikia kwenye viwanja vya Chinangali, Dodoma.
Washindi hao walikabidhiwa makombe yao na Naibu waziri, ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius John Ndejembi kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Mbali ya vikombe, washindi pia walikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 6.5 kwa washindi wa kwanza huku washindi wa pili wakikabidhiwa hundi ya Shilingi milioni 3 kila mmoja.
Pia kulikuwa na zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na ile ya mchezaji mwenye thamani kubwa MVP ambapo Alinani Endrew wa Dar es Salaam alishinda kwa upande wa wanaume na Noela Renatus pia wa Dar es Salaam alishinda kwa upande wa wanawake.

Benki ya CRDB imetumia Shilingi milioni 300 kudhamini mashindano hayo. Mbali ya benki ya CRDB kuwa wadhamini wakuu, wadhamini wengine walikuwa GSM, Azam TV, Sanlam, Tulia Trust, PSSF, EFM na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Nsekela alisema kuwa mbali ya kuchangia maendeleo ya michezo kupitia mashindano hayo, benki ya CRDB imesaidia vijana kwa kutoa fursa za ufadhili wa masomo na kuchangia katika sekta ya elimu.
Alisema kuwa wamekuwa wakipokea salamu nyingi za pongezi kutoka wa viongozina watu mbalimbali ikiwa ni ishara ya kuonyesha kuwa maamuzu yao ya kudhamini mashindano hayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Nsekela pia alisema kuwa benki ya CRDB itaendelea kuwekeza katika mchezo wa mpira wa kikapu na kuhakikisha kuwa unakua mmoja kati ya michezo yenye kubadili maisha ya vijana kiuchumi ili kuendana na kauli mbiu yake ya “Ni Zaidi ya Game Ni Maisha”.
Alisema kuwa Menejimenti ya benki ya CRDB imedhamini mashindano hayo kwa kujua kuwa yana tija kwani inatoa fursa kwa vijana mbali na maendeleo ya michezo nchini.
Ndejembi alisema kuwa mchezo wa mpira wa kikapu una fursa nyingi mbali ya kukuza vipaji, kwani pia umewekeza katika elimu.
Hamasa imekuwa kubwa sana na kila kona ya nchi hususan hapa Dodoma watu wanazungumzia CRDB Bank Taifa Cup kuanzia masokoni, maofisini, mitaani hadi Bungeni,” alisema Ndejembi.
Alisema kuwa mashindano ya mwaka huu yametoa funzo kwa wachezaji na kuwataka wasisubiri fursa za kwenda NBA na ligi nyingine kubwa kwani wanatakiwa kuzifuata huko na kuonyesha vipaji vyao.
Aliongeza kuwa idadi ya mashabiki imekuwa chachu ya maendeleo ya mchezo huu na kutoa wito kwa TBF kuendeleza mchezo huu mpaka ngazi za shule za msingi na sekondari.
No comments:
Post a Comment