Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 11 October 2021

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA BENKI YA DCB YANG'ARA

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Dk. Amina Abdul (katikati) akikata keki katika hafla ya kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika makao makuu mwa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Sheria na Katiba, Regina Mduma, Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Ndalahwa, Mkurugenzi wa Viashiria Hatarishi, Doreen Joseph na Mkurugenzi wa Biashara, Zacharia Kapama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (wa pili kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi 910,000 kwa washindi wa pili kwa tawi lililofanya vyema katika wiki ya huduma kwa wateja, Tawi la Uhuru katika hafla ya kuhitimisha wiki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wa tatu kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya DCB, Dk. Amina Abdul.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (wa pili kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Dk. Amina Abdul (wa pili kulia) wakikabidhi kikombe kwa washindi wa kwanza wa tawi lililofanya vizuri katika wiki ya huduma kwa wateja, Tawi la Magomeni na Victoria katika hafla ya kuhitimisha wiki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni, Meneja wa tawi la Magomeni, Al-Amin Lwano na Meneja wa Tawi la Victoria, Aziza Kizigha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (katikati) na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Dkt. Amina Abdul (wa pili kulia) wakikabidhi mfano wa hundi shilingi 4,200,000 kwa washindi wa kwanza wa tawi lililofanya vyema katika wiki ya huduma kwa wateja, Tawi la Magomeni na Victoria wakati wa hafla ya kuhitimisha wiki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Meneja wa Tawi la Victoria, Aziza Kizigha, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Rahma Ngassa na Meneja wa Tawi la Magomeni, Al-Amin Lwano.
Ofisa Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya Biashara ya DCB, Constantine Mtumbuka (katikati), Ofisa wa Magereza, Florian Rutha (kushoto) na Muhamasishaji wa Vikundi vya Kijamii, Asha Pembe wakikata keki kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja wa benki hiyo katika hafla iliyofanyika katika Tawi la DCB Ukonga, Dar es Salaam.
Wakiwa na nyuso za uchangamfu ni wafanyakazi wa Benki ya DCB wa Tawi la Mabibo jijini Dar es Salaam wakijinasibu kuendelea kutoa huduma Bora kwa wateja wao muda wote hata kama si katika kipindi cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Biashara ya DCB Tanzania, Fortunata Benedict (wa tano kushoto), akiungana na wafanyakazi na wateja wa Tawi la DCB Uhuru jijini Dar es Salaam, kukata keki ikiwa ni moja ya shamrashamra ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja jijini humo mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi wa Sheria wa Benki ya Biashara ya DCB na Katibu wa Kampuni, Regina Mduma (wa pili kulia), na Meneja wa Benki hiyo Tawi la Mabibo Dorah Kalinga (kushoto), wakikata keki pamoja na wateja wao kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja tawini hapo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment