Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 7 October 2021

BALOZI MULAMULA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA FAO, ROMA - ITALIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Dkt. Qu Dongyu. Mazungumzo hayoyamefanyika Makao Makuu ya Shirika hilo yaliyopo Roma, Italia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Dkt. Qu Dongyu. Wengine katika picha ni ujumbe wa Balozi Mulamula na Dkt. Qu wakifuatilia mazungumzo hayo
Balozi wa Tanzania Nchini Italia Balozi Mahmoud Kombo (kulia) akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ulaya na Amerika Bw. Gerald Mbwafu (katikati) pamoja na Katibu wa Waziri Bw. Charles Mmbando wakifuatilia mazungumzo ya Balozi Mulamula (Mb) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa FAO (hawako pichani).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa amesimama katika nembo ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) iliyopo katika makao makuu ya Shirika hilo yaliyopo Roma Italia,kabla ya kukutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dkt. Qu Dongyu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Italia Balozi Mahmoud Kombo wakiwa katika picha ya pamoja Katika nembo ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) iliyopo katika makao makuu ya Shirika hilo yaliyopo Roma Italia, kabla ya kukutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dkt. Qu Dongyu.
  • FAO YAISHAURI TANZANIA KUHUSU MAZAO YA KILIMO KATIKA SOKO LA KIMATAIFA
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limeishauri Tanzania kuweka kipaumbele katika zao moja la kilimo litakaloitambulisha Tanzania Kimataifa ili kuweza kupenya kirahisi katika soko la Kimataifa la mazao ya kilimo.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Dkt. Qu Dongyu alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula(Mb) mazungumzo yaliyofanyika katika makao makuu ya Shirika hilo Roma,Italia.

Dkt. Qu Dongyu ameongeza kuwa Tanzania ina mazao muhimu na mengi ya kilimo ambayo yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza pato la Taifa lakini changamoto kubwa ni namna ya kupenya katika soko la kimataifa kutokana na kukosa zao la utambulisho na kwamba Shirika hilo FAO iko tayari kusaidia ujuzi na kuijengea uwezo Tanzania kufikia lengo hilo .

Dkt. Qu Dongyu ameongeza kuwa kwa sasa FAO imeanzisha jukwaa maalum la kuwawezesha wanawake na vijana kunufaika na sekta ya kilimo kutokana na utafiti kuonesha kuwa wanawake wengi katika nchi zinazoendelea wanajihusisha na kilimo.

Katika mazungumzo hayo Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Libearata Mulamula amesema Tanzania imeupokea ushauri wa FAO na kwamba itaufanyia kazi ili kuiwezesha Tanzania kutambulika na kunufaika katika soko la Kimataifa la mazao ya kilimo ili kuwawezesha wakulima kujikomboa kiuchumi kwa kuongeza pato la kaya na hivyo kuinua uchumi wa Tanzania.

Ameongeza kuwa Tanzania imejipanga kikamilifu kunufaika na mpango wa Shirika la chakula na Kilimo la Umoja wa Matiafa (FAO) wa kuanzisha jukwaa maalum la kuwawezesha wanawake na vijana kunufaika na sekta ya kilimo kutokana na utafiti kuonesha kuwa wanawake wengi katika nchi zinazoendelea wanajihusisha na kilimo

Balozi Mulamula yuko Roma,Italia kushiriki Mkutano wa tatu wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi za Afrika na Italia pamoja na kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa amani.

No comments:

Post a Comment