Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Thursday, 7 October 2021
BENKI YA TCB YAZINDUA WIKI YA MTEJA YAAHIDI KUFANYA MAKUBWA KWA WATEJA WAKE
BENKI ya Biashara Tanzania (TCB) imesema hatua ya serikali kuweka mifumo imara ya kifedha imezidi kuziboresha huduma za kifedha nchini ikiwemo kuongeza namba ya watu wanaotumia mifumo rasmi ya kifedha.
Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha wiki ya huduma Kwa wateja Mkurugenzi mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi amesema nia yao ni kutoa huduma hasa kuwapa fursa wateja wadogo wadogo ambao ndiyo azma ya Serikali na Benki hiyo.
Moshingi amesema kuwa nia yao nikusogeza huduma rafiki kwa wateja wake ili kuhakikisha kuwa kila Mtanzania wa hali ya chini anatumia benki hiyo kwa ajili ya uendeshaji wa biashara zao katika nyanja tofauti.
Kwa upande wao baadhi ya wateja na watumiaji wa mifumo ya kibenki wamesema kitendo cha baadhi ya taasisi kuanzisha huduma za kuwajali wastaafu imezidi kuongeza weledi hivyo wameishukuru Benki ya TCB kwakuendelea kuwaamini nakuwawezesha kupata mikopo kwa wakati na kwa masharti rafiki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment