Mikopo hiyo itatolewa kwa kiwango cha riba isiyozidi asilimia 10% kwa mwaka. Wanufaika wa mikopo hii ya riba nafuu ni wakulima, wauzaji wa pembejeo, watoa huduma, wajasiriamali na wasindikaji wadogo na wa kati wanaojishughulisha na shughuli zote katika sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi.
Zaidi ya Shilingi Bilioni 100 zimetengwa kwaajili ya kutoa mikopo nafuu kwenye sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi.
Benki ya NMB inachukua hatua hii ili kupanua wigo wa wadau wengi katika sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi kupata mikopo yenye riba nafuu ambayo itaongeza tija katika shughuli zao za kiuchumi.
Mteja sasa ataweza kuwa na unafuu wa gharama ya mkopo na hivyo kuweza kujitengenezea faida zaidi. Faida hiyo inaweza kutumika kuongeza uzalishaji wa chakula, malighafi za viwanda na kuchagiza maendeleo ya viwanda nchini.
Ni matarajio ya benki ya NMB kuwa wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo na wa kati katika tasnia hii wataitumia fursa hii adhimu kujipatia mikopo yenye gharama nafuu na kujiongezea kipato ili kujenga uchumi wa nchi.
Benki itazingatia masharti ya utoaji wa mikopo hii nafuu kwa kuzingatia taratibu za ukopeshaji ikiwemo kiwango cha juu cha mkopo cha TZS 1 Bilioni kwa mkopaji mmoja. Mkopaji huyu anaweza kuwa mtu binafsi, chama cha ushirika, kampuni au taasisi yeyote itakayokidhi masharti ya ukopeshaji.
Benki inatoa wito kwa walengwa kuwasiliana na mtandao wake wa zaidi ya matawi 225 yaliyo enea nchi nzima ili kuweza kupata huduma za mikopo hii ya riba nafuu.

No comments:
Post a Comment