Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Sunday, 7 March 2021

BENKI YA NBC YADHAMINI MAONESHO YA WAFANYABIASHARA WANAWAKE TANZANIA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi (Uwekezaji) Kitila Mkumbo (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa wafanyabiashara wanawake yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC yenye kauli mbiu mwanamke miliki kiwanda kwa uchumi endelevu. Maonesho yalizinduliwa na Waziri huyo katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Mussa Mwinyidaho.
Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Mussa Mwinyidaho akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonesho ya wafanyabiashara wanawake Tanzania yaliyodhaminiwa na Benki hiyo ambapo katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi (Uwekezaji) Kitila Mkumbo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi (Uwekezaji) Kitila Mkumbo (katikati) akipokea zawadi ya kifungashio kilichotengenezwa na wajasiriamali wa kitanzania wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonesho ya wafanyabishara wanawake Tanzania yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC kutoka kwa Mkurugenzi wa Chama cha Wafanyabiashara Tanzania (Tabwa), Noreen Mawalla. Kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Mussa Mwinyidaho.
Baadhi ya wanawake waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakifurahia jambo kutoka kwa mgeni rasmi.
Picha ya pamoja.

Serikali imewataka wanawake kuchangamkia fursa zinazotolewa katika mikoa wanayoishi ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili hasa kwenye swala zima la mitaji.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubumgo wakati alipoalikwa kuwa Mgeni rasmi na kuzindua maonyesho ya biashara za wanawake Tanzania yaliyodhaminiwa na Benki ya Taifa ya bishara NBC,kwa lengo mahususi la kuwainua wanawake kiuchumi yanayofanyika Mlimani City kwa siku tatu mfululizo.

Waziri Mkumbo amesema Serikali kwa kutambua umuhimu na mchango wa maendeleo kwa wanawake kwa Taifa, letu na Serikali inayoongozwa na jemedali wetu Rais John Pombe Magufuli wameanzisha dirisha maalumu la mikopo kwa halmashauri zote nchini kwa ajili ya kuwainua wanawake na vijana.

"Tunatambua jitihada zenu na malengo yenu lakini Serikali tunatoa wito kwa wanawake wote nchini kuchangamkia fursa zinazotolewa kupitia mikoa yao ziweze kuwasaidia kwenye changamoto zinazowakabili,” amesema Waziri Mkumbo.

Waziri huyo pia ameishukuru Benki ya Taifa ya Biashara NBC ambayo ndio mdhamini mkuu wa maonesho hayo kwa uzalendo walioufanya kutambua kuwa hakuna maendeleo bila wanawake na kulibeba hili ili wanawake waweze na vijana waweze kwenda sawa na spidi ya uchumi wa kati na kuzitaka Taasisi nyengine kuiga mfano huo kwani utaleta matokeo nyanya katika sekta ya uwekezaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chama cha Wafanyabiashara Tanzania (Tabwa), Noreen Mawalla aliiomba Serikali kuwasaidia majengo ya wazi ili wanawake wafanyie biashara zao katika mazingira mazuri na salama yatakayowawezesha kulipa kodi kwa wakati.

Nae Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Mussa Mwinyidaho katika uzinduzi huo leo, amemwambia Waziri kuwa lengo kuu la udha mini wa benki hiyo kwa maonesho hayo ya wanawake wafanya biashara tanzania ni kuwawezesha wajasiliamari wadogo na wa kati ambao ndiyo walengwa wakuu wa maonesho haya.

NBC ni Benki inayo wajali wateja wake na watanzania wote kwa ujumla hivyo ili waweze kuwa wafanyabiashara bora nilazima wapate elimu ya kifedha hivyo tunawakaribisha NBC waje wapate elimu pia kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo alisema mwinyidaho.

No comments:

Post a Comment