Takribani wachezaji 150 wa gofu kutoka sehemu mbali mbali hapa nchini wanatarajia kuchuana vikali kwenye mashindano ya kila mwaka maarufu kama Waitara Golf Tournament, yanayodhaminiwa na kinywaji cha Johnnie Walker (JW) kinachosambazwa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL)
Mwaka jana, mashindano haya yanayojizolea umaarufu mkubwa, yalidhaminiwa pia na kampuni ya SBL kupitia bia yake ya Serengeti Lite.
Akitangaza udhamini huo mbele ya waandishi wa habari, mkurugenzi wa masoko wa SBL Mark Mugisha alisema udhamini wa JW kwenye mashindano hayo unalenga kukuza na kuendeleza mchezo wa gofu.
“SBL kupitia kinywaji cha kimataifa cha Johnnie Walker inayofuraha kuwa mdhamini wa mashindano ya Waitara Golf Tournament kwa mwaka huu. Udhamini huu unaonyesha nia yetu ya kusaidia maendeleo ya michezo hapa nchini,” alisema Mark.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa mashindano hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka kuanzia mwaka 2006, na hivyo mashindano yaliyoanza muda mrefu zaidi hapa Tanzania na kuongeza kuwa JW inayofuraha kuwa sehemu ya mashindano hayo makongwe.
“Wakati tukishereheka miaka 200 tangu kuanza kutengenezwa kwa JW ambayo kwa sasa ni wisky namba moja ulimwenguni, tunayofuraha kusafiri katika miaka yote hii tukiendelea kuwa imara na katika ubora ule ule,” alisema.
Johnnie Walker ni moja kati pombe kali zenye ubora wa hali ya juu na hadhi ya kimataifa. Kinywaji hiki kina jumla ya aina tano ambazo zimeshinda tuzo za ubora wa kimataifa. Aina hizo ni pamoja na JW Red Label, JW Black Label, JW Green Label, JW Gold Label, na JW Blue Label kila moja ikiwa na historia yake ya kipekee.
Kwa upande wake mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Lugalo Bregedia Generali mstaafu Michael Luwongo aliishukuru SBL kupitia JW kwa kukubali kudhamini mashindano hayo na kuyataka makampuni mengine kujitokeza kusaidia mchezo wa gofu.
“Tunaishukru sana kampuni ya SBL kwa muendezo wao wa kufadhili mashindano hay ana mchezo wa gofu kwa ujumla. Kwa sasa tunaweza kusema SBL ndiyo mdhamini mkubwa wa mashindano haya,” alisema Bregedia Jenerali Luwongo.
No comments:
Post a Comment