Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 9 October 2020

RAIS MAGUFULI, RAIS CHAKWERA WAWEKA JIWE LA MSINGI KITUO CHA MABASI MBEZI

RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus Chakwera wameweka jiwe la msingi katika kituo kipya cha mabasi Mbezi Luis Jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kuweka jiwe la msingi, Rais Dkt. Magufuli ametoa maagizo, kwa waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kabla ya tarehe 30 Novemba 2020, vinginevyo mkandarasi atakatwa Pesa kwa kuchelewesha mradi.

Kituo hicho kinatarajiwa kuwa na uwezo wa kubeba mabasi 1,000 na teksi 280 kwa siku, Pia kutakuwa na maeneo ya bodaboda na bajaji na na eneo la mamalishe na babalishe.

Mbali na kuweka jiwe la msingi katika kituo cha mabasi mbezi Luis, Rais Chakwera pia ametembelea maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), Kampuni ya Huduma za Kontena Bandarini (TICTS), Kituo cha Mizigo cha Malawi (Malawi Cargo Center) pamoja na Bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera mara baada ya kumpokea katika eneo la ujenzi wa stendi mpya ya Mbezi Luis Jijini, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera wakiwa wamesimama huku wakiimba nyimbo za Taifa za mataifa yote mawili kabla ya kuanza rasmi kwa shughuli ya uwekaji wa jiwe la msingi katika maradi wa ujenzi wa stendi mpya ya Mbezi Luis Jijini, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika eneo la maradi wa ujenzi wa stendi mpya ya Mbezi Luis Jijini, Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera kuongea na wananchi kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa stendi mpya ya Mbezi Luis Jijini, Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akimuonesha Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera mradi wa ujezi wa Reli ya Kisasa (SGR) wakati alipotembelea mradi huo Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera akiongea na wananchi (hawapo pichani) waliojitokeza wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa SGR jijini Dar es Salaam. Kushoto mwa Rais Chakwera ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Bw. Masanja Kadogosa akifuatiwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwele pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi.
Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera pamoja na mkewe Mama Monica Chakwera wakipokea zawadi kutoka kwa uongozi wa Kituo cha Mizigo cha Malawi (Malawi Cargo Center) wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa SGR jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa, Dkt. Lazarus Chakwera pamoja na mkewe Monica Chakwera wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya kuhudumia Makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS), Bw. Horace Hui mara baada ya kutembelea kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa, Dkt. Lazarus Chakwera akiongea na wananchi pamoja na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati alipotembela Bandari ya Dar es Salaam jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment