Mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam na Arusha, ni utekelezaji wa maagizo ya Benki Kuu (BoT) kuhakikisha mawakala wa benki hawawi sehemu ya kutakatisha fedha zinazopatikana kwa njia zisizo halali.
Akizungumza wakati wa semina hiyo, Meneja Mwandamizi wa NMB Kitengo cha Wakala, Bw. James Manyama alisema ili mawakala hao kutotumika vibaya hawana budi kuzingatia sheria na kanuni za fedha zinazosimamiwa na Benki Kuu ili kushirikiana na Serikali katika kukomesha vitendo hivyo.
Mawakala kutoka Manispaaa ya Temeke wakiwa katika mafunzo ya jinsi wanavyoweza kuzuia utakatishaji fedha. |
Christine Mwidunda, ambaye ni Meneja wa Mawakala NMB, alisema vyanzo vya fedha haramu ni kama vile ukwepaji wa kodi, biashara zilizopigwa marufuku zikizemo dawa za kulevya, usafirishaji wa silaha na binadamu, ugaidi na utekaji n.k.
Christine Mwidunda, akitoa mafunzo kwa Mawakala jijini Arusha. |
Mawakala wakiwa na vyeti walivyopewa baada ya kuhitimisha mafunzo ya namna gani wanaweza kuzuia utakatishaji fedha. |
Benki ya NMB imepanga kutoa mafunzo haya kwa mawakala wake wote 7,700 ambao wametapakaa nchi nzima ifikapo mwezi Oktoba, 2020.
No comments:
Post a Comment