Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 16 October 2019

WAFANYABIASHARA KUMI (10) WA NMB BUSINESS CLUB WAPAA KUSHIRIKI CANTON FAIR CHINA

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard (wa pili kulia), akikabidhi mfano wa tiketi ya kwenda China kwa Mfanyabiashara kutoka Musoma mkoani Mara, Oliver Kisamba (wa pili kushoto) wakati wa hafla ya kuwakabidhi tiketi wafanyabiashara kumi (10) kwa ajili ya kwenda China kushiriki kwenye maonyesho ya 125 ya biashara yatakayofanyika nchini humo. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB Idara ya Biashara, Theresia Mayanie na wa kwanza kulia ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha wafanyabiashara wadogo, Beatrice Mwambije.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard (wa tatu kulia) akiwakabidhi mfano wa tiketi wafanyabiashara kumi (10) waliodhaminiwa na Benki ya NMB kwenda nchini China kwa ajili ya kushiriki maonyesho ya biashara nchini humo.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB, Donatus Richard akizungumza na wafanyabiashara kati ya kumi waliofadhiliwa na Benki ya NMB kwenda nchini China kwa ajili ya kwenda kushiriki maonyesho ya biashara yanayaotarajia kuanza wiki hii nchini humo wakati wa hafla ya kuwakabidhi tiketi jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Wafanyabiashara kumi (10) wanachama wa Klabu za Biashara za Benki ya NMB (NMB Business Club), wameondoka nchini kwenda China, kushiriki Maonesho ya 125 ya Canton Fair 2019, yanayofanyika wiki hii mjini Guangzhou, ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kibiashara ya siku 10.

Tiketi za safari ya wafanyabiashara hao (kwenda na kurudi), malazi, chakula na kila kitu, vimegharamiwa na Benki ya NMB, ambayo iliwataka kuitumia fursa hiyo vema kwa kwenda kujifunza namna ya kuboresha biashara, kukuza mitaji na kuchangia uchumi wa taifa.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wafanyabiashara hao kutoka Kanda mbalimbali za klabu zao nchini, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB, Donatus Richard, (Head of Business Banking) aliwataka kuwa mabalozi wema NMB wakiwa China na kutumia vema elimu watakayopata kupitia maonesho watakayoshiriki.

“Ni matumaini yetu kwamba mtaitumia vizuri safari hii kujifunza fursa mbalimbali za kibiashara zikiwemo za uwekezaji wa viwanda ili kuendana na kasi ya Tanzania ya Viwanda inayochakatwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.

“Kufanya hivyo kutawasaidia kuongeza mbinu katika nyanja mbalimbali, ikiwemo kujua kwa namna gani mnaweza ushirikiana kufanya biashara kimataifa, hatua ambayo itawanyanyua kiuchumi,” alisema Richard huku akiwataka kurejea wakiwa bora zaidi kimbinu katika kukuza mitaji yao.

Kwa niaba ya NMB, Donatus akawasistiza wafanyabiashara hao kuwa, furaha yao kama taasisi kinara ya fedha nchini itakuwa ni kushuhudia mapinduzi chanya ya kimaendeleo kupitia elimu watakayopata kupitia ziara na maonesho watakayoshiriki China.

Akitaja vigezo vilivyotumika kupata wafanyabiashara hao 10 kutoka miongoni mwa wanachama zaidi ya 200,000 kote nchini, Richard alisema ni pamoja na rekodi nzuri za marejesho ya mikopo na nguvu ya ushawishi ya mwanachama kuongeza wanachama/wateja wapya katika NMB.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa NMB Business Club wilaya ya Ilala, Award Mpandilah, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kamuni ya Mpandilah General Supplies Ltd, aliishukuru NMB kwa fursa waliyowapa, ambayo ana uhakika inaenda kubadili mifumo yao kibiashara.

Alibainisha ya kwamba, ziara ya siku 10, inayoambatana na ushiriki wa Maonesho ya Canton Fair 2019, vitawaongezea elimu na kuwatia chachu ya mafanikio kibiashara na kwamba watarejea wakiwa wamejenga chaneli za ushirikiano na wafanyabishara wa nchi hiyo.

“Ni fursa ambayo inatamaniwa na kila mtu aliye na kiu ya maendeleo. Tunaishukuru NMB kwa nafasi waliyotupatia na tunaahidi kuitumia vema kuhakikisha tunapiga hatua za haraka kimaendeleo ya mfanyabiashara mmoja mmoja, benki inayotuhudumia na taifa kwa ujumla,” alisema Mpandilah.

No comments:

Post a Comment