- Hospitali binafsi, zahanati, vituo vya afya, wasambazaji huduma za matibabu kupata mikopo yenye bei nafuu
- Inatarajiwa kuboresha utoaji huduma za afya nchini
Huduma hii mpya ni matokeo ya ushirikiano kati ya Benki ya NMB na shirika la Stichting Medical Credit Fund (MCF) ambapo NMB itatoa mikopo kuanzia Sh Milioni 2 hadi Bil 5 wakati MCF inatoa dhamana ya asilimia 50 katika mikopo yote.
Wafaidika wa Mkopo wa Afya ni hospitali binafsi, vituo vya afya na zahanati, maduka ya dawa na wasambazaji dawa ili kuwezesha, kuiinua na kuboresha biashara za huduma za afya nchini.
Aidha, Benki ya NMB ndio benki ya kwanza nchini Tanzania kuingia katika ushirikiano kama huo na MCF nia ikiwa kujenga uwezo Sekta ya Afya.
Kwa pamoja NMB na MCF watashirikiana kutekeleza ufadhili wa huduma ya afya, kupanua na kuimarisha ubora wa utoaji wa huduma hiyo muhimu kwa wananchi.
Huduma hii itawawezesha watoa huduma ya afya kupata fedha pamoja na kupata utaalum wa kiufundi, ambao utasaidia kutambua wauzauji na vifaa vya matibabu bora pamoja na upatikanaji wa vifaa vya tiba kwa ajili ya uboreshaji wa huduma zao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Mkuu wateja binafsi, biashara ndogo na za kati Filbert Mponzi alisema, huduma hiyo ya mikopo imefika kwa wakati mwafaka na utachangia kuongeza upatikanaji wa huduma nafuu za afya na kujenga mifumo endelevu kwasababu upatikanaji wa mitaji unakuwa rahisi zaidi.
"Hii ni hatua nyingine kubwa kwa Benki ya NMB leo. Kuna fursa nyingi katika sekta ya afya nchini na sisi kama NMB, tumeliona hili na tumejikita kuwapa nafasi hospitali, vituo vya afya wasambazaji wa vifaa vya tiba kujiendeleza. Tunaimani huduma hii itachangia kwa kiasi kikubwa katika upatikanaji mkubwa wa utoaji huduma za afya za bei nafuu, "alisema Mponzi.
Itakumbukwa, Benki ya NMB imepigiwa kura kuwa benki nzuri zaidi nchini kwa miaka saba mfululizo na tuzo za kifahari za kimataifa za Euromoney; vilevile ndio benki inayoongoza katika kufadhili biashara ndogo na za kati kwa sekta mbalimbali.
Mkurugenzi wa MCF Tanzania, Dk. Heri Marwa alisema kuanza utekelezaji wa huduma hiyo mpya ni muhimu katika kutimiza malengo ya MCF ya kuhakikisha watanzania wengi wapata huduma nafuu za afya na tiba.
"Upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya uwekezaji ni changamoto kubwa katika nchi nyingi za Kiafrika na inazuia utoaji huduma nafuu za afya hususan tukiangalia mifumo endelevu ya afya.Kwa huduma hii tunafurahi kwamba hospitali nyingi binafsi, vituo vya afya vitapata na uwezo wa kuwekeza kwenye vifaa vya afya vya kisasa, na tunafurahi kushirikiana na benki bora nchini Tanzaniakufanikisha upatikanaji wa mitaji ya biashara nchini,” alisema Dk. Heri Marwa.
Kuhusu NMB
Benki ya NMB Plc. (“NMB”) ni benki kamili ya kibiashara iliyosajiliwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kupitia idara zake 4: Wateja Wadogo, Wateja Wakubwa, Kilimo Biashara na Fedha, NMB inatoa huduma za kifedha na bidhaa kwa wateja wadogo, wakulima, SME, mashirika, taasisi na Serikali.
Benki ina matawi 299, zaidi ya mawakala 6,000 na zaidi ya ATM 800 nchi nzima na ipo katika wilaya zote za Tanzania. NMB ina zaidi ya wateja milioni 3 na imeajiri zaidi ya wafanyakazi 3,600. Imesajiliwa katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) na wabia wake wakubwa ni Rabobank wenye hisa za asilimia 34.9 na Serikali ya Tanzania iliyo na hisa 31.9.
Tuzo ya ubora ya Euromoney iliichagua NMB kuwa “Benki Bora Tanzania” kwa miaka 7 mfululizo kuanzia 2013-2018. Iliipa tuzo ya Mshirika Bora wa Kifedha Afrika kwa benki zinazofanya kazi na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) kwa Kundi la Benki ya Dunia na pia ilipata tuzo ya Benki Bora ya Wateja Wadogo na Kibiashara Tanzania iliyotolewa na Jarida la Mabenki Afrika Mashariki. Kwa maelezo zaidi kuhusu NMB na huduma zake, tafadhali tembelea tovuti yetu: www.nmbbank.co.tz
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:
Rahma Mwapachu,
Kaimu Mkuu wa Mawasiliano,
Benki ya NMB Plc.
Barua pepe: Rahma.Mwapachu@nmbtz.com
Barua pepe: Rahma.Mwapachu@nmbtz.com
No comments:
Post a Comment