Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 17 September 2019

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AZINDUA RADA MBILI ZA KUONGOZEA NDEGE ZA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE NA UWANJA WA NDEGE WA KIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria uzinduzi wa Rada mbili za kuongozea Ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA katika Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Viongozi wengine kwenye picha ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari pamoja na Balozi wa Ufaransa hapa nchini Fredrick Clavier.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Rada mbili za kuongozea Ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA katika Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) Hamza Johari kuhusu utendaji kazi wa Rada hiyo mpya ya kuongozea ndege.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Ufaransa hapa nchini Fredrick Clavier mara baada ya kuzindua mfumo wa Rada za kuongozea Ndege katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments:

Post a Comment