Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 5 September 2019

BIDHAA YA UNGA WA NGANO YA AZAM SASA KUPATIKANA KATIKA VIFUNGASHIO VIPYA

Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Said Bakhresa Group, Hussein Sufian (kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo Ahmed Jaruan, wakionyesha waandishi wa habari muonekano mpya wa vifungashio vya unga wa ngano wa Azam ujulikanao kama Ngano Bora, ikiwa ni mkakati wa kulinda ubora na kutambulisha bidhaa zake kwa wateja.

Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Said Bakhresa Group, Hussein Sufian akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaaam (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa muonekano mpya wa vifungashio vya unga wa ngano wa Azam ujulikanao kama Ngano Bora, ikiwa ni mkakati wa kulinda ubora na kutambulisha bidhaa zake kwa wateja.Wengine pichani ni Maofisa Waandamizi wa kampuni hiyo

Uongozi wa kampuni ya kutengeneza vyakula inayomikiliwa na makampuni ya Said Salim Bakhresa &Ltd, inayozalisha unga bora wa ngano wenye jina la kibiashara la Azam, imetangaza kubadilisha muonekano wa bidhaa yake maarufu ya unga wa ngano unaojulikana kwa chapa ya Ngano Bora.

Muonekano mpya wa kifungashio (mfuko) wa bidhaa hii umeboreshwa ili kuwapatia wateja wake kuitambua kwa urahisi na kuweza kuitofautisha na bidhaa zenye vifungashio vinavyofanana nayo.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni hiyo,Hussein Sufian , amesema kumekuwepo na wazalishaji ambao wanaiga na kubadilisha rangi za muonekano wa bidhaa zao zifanane na bidhaa za AZAM, hali ambayo imekuwa ikiwachanganya wateja kwenye masoko kutambua bidhaa za kampuni hiyo.

Alisema kutokana na kubadilisha vifungashio, wateja wa Ngano Bora, unaotengenezwa na AZAM kwa sasa wataweza kutambua bidhaa hizo kwa urahisi pia ametoa tahadhari kwa wazalishaji wasio waaminifu ambao wamekuwa wakiiga muonekano wa bidhaa za kampuni hiyo kuacha kufanya hivyo kwa kuwa wanavunja sharia na tayari wameishatoa taarifa kwa mamlaka mbalimbali,watakaokamatwa kwa kufanya udanganyifu huu watachukuliwa hatua za kisheria.

Aidha kampuni imetoa tahadhari kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa wakitumia vifungashio vya bidhaa za kampuni hiyo zilizotumika na kujaza bidhaa nyingine na kuziuza kwa wateja kama bidhaa za kampuni ya AZAM.

Sufian alisema kampuni inapenda kuwahakikishia wateja wake kuwa itaendelea na ubunifu na uzalishaji wa bidhaa zenye kiwango cha juu ubora kukidhi matakwa ya wateja wote nchini na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment