Afisa Mawasiliano wa Mradi wa TLED, Jemima Michael akizungumza wakati wa maonyesho hayo. |
Akizungmza katika Maonesho ya Biashara ya 43 ya kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam Michael amefafua mradi huo ni wa miaka mitano chini ya ufadhili wa Global Affairs Canada (GAC) na ulianza Aprili mwaka 2015 hadi Machi mwaka 2020.
"Ni mradi wenye lengo la kukabilana na changamoto za kibiashara ambazo wajasiriamali wadogo na wakati wanakutana nazo hasa upatikanaji na ukuaji wa masoko katika sekta ya biashara ya kilimo,"amesema.
Ameongeza nia ya TLED ni kuoa wajasiamali wanapiga hatua katika shughuli zao za kibiashara na kiuchumi n kuboresha utoaji wa ajira kutokana na maendeleo na huduma za kifedha kwa wajasiriamali katika mikoa sita nchini.
Ameitaja mikoa hiyo ambayo imefaidika mradi huo wa TLED ni Shinyanga, Mwanza, Lindi, Mtwara, Iringa na Njombe huku malengo mahususi ni kuhakikisha mnufaikaji wa mradi huo anapatiwa elimu na ushauri kutoka kwa timu ya washauri wakuu (wanaojitolea) na wafanyakazi wa mradi.
Pia amesema TLED inahakikisha wanufaikaji wa mradi huo wanaunganishwa na soko la biashara zao, upatikanaji wa teknolojia na upatikanaji wa fedha kwaajili ya kuendeshea biashara hizo.
Akifafanua zaidi malengo mengine ya mradi huo ni kuwafikia wajasiriamali 1,760 mpaka ukomo wa mradi huo, ambao kwa sasa mradi huo umefikia wajasiriamali 1,361 sawa na asilimia 77 ya walengwa.
Kuhusu maonesho hayo, Michael amesema wametumia fursa hiyo kuwapa fursa wajasiliamali kujifunza kwa kuona wenzao wanafanya nini na kuzitangaza biashara zao kimataifa kupitia jukwaa hilo la maonesho ya biashara.
Kwa upande wake Mjasiriamali wa kutengeneza mikoba asili kutoka mkoani Shinyanga ameushukuru mradi wa TLED kwa kumpa fursa ya kushiriki maonesho hayo.
No comments:
Post a Comment