Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 21 June 2019

WENGINE WAWILI WAJISHINDIA TIKETI ZA TIGO KUSHUHUDIA MICHUANO AFCON

Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Tigo Woinde Shisael (kati kati) akiongea na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuwakabidhi stakabadhi ya kusafiria (boarding pass) washindi wa droo ya pili ya promosheni ya Soka la Afrika watakaokwenda Misri kushuhudia michuano ya mataifa ya Afrika. Kushoto ni Sanga Massawe ambaye ni mshindi kutoka Moshi na kulia ni Emmanuel Mushi mshindi kutoka Dar es Salaam.
Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Tigo Woinde Shisael akimkabidhi Sanga Massawe ambaye ni mshindi wa droo ya pili ya promosheni ya Soka la Afrika stakabadhi ya kusafiria (boarding pass) kwa ajili ya kwenda kushuhudia michuoano ya Mataifa ya Afrika yanayofanyika nchini Misri baada ya kuibuka mshindi kwenye promosheni hiyo inayoendelea.
Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Tigo Woinde Shisael akimkabidhi Emmanuel Mushi ambaye ni mshindi wa droo ya pili ya promosheni ya Soka la Afrika stakabadhi ya kusafiria (boarding pass) kwa ajili ya kwenda kushuhudia michuoano ya Mataifa ya Afrika yanayofanyika nchini Misri baada ya kuibuka mshindi kwenye promosheni hiyo inayoendelea.
Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Tigo Woinde Shisael (kati kati) akiwa na washindi wa promosheni ya Soka la Afrika Emmanue Mushi kushoto na Sanga Massawe (kulia) muda mfupi baada ya kukabidhiwa bendera ya Taifa kwa ajili ya kwenda kuishangia timu ya Taifa, Taifa Starts kwenye mashindano ya Mataifa ya Afrika yanayofanyika nchini Misri.
Kupitia droo ya pili ya promosheni ya SOKA LA AFRIKA, kampuni ya Tigo imewatangaza washindi wengine wawili na kuwakabidhi tiketi za kwenda kushuhudia michuano ya Mataifa ya Afrika yanayofanyika nchini Misri na kufanya idadi ya washindi kuwa watano.

Washindi walioshinda tiketi katika droo ya pili ni Sanga Massawe kutoka Moshi Kilimanjaro na Emmanuel Mushi kutoka Dar es Salaam.

Mapema wiki iliyopita, Tigo iliwakabidhi tiketi washindi watatu katika droo ya kwanza ya promosheni hiyo. Washindi wa droo ya kwanza ni Kalaghe Rashid na Godfrey Muta kutoka Dar es Salaam na Rehema Kassim kutoka Tanga.

Kupitia Promosheni ya Soka la Afrika, wateja wa Tigo wanayo nafasi ya kujishindia safari ya kwenda Misri kushuhudia michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika pamoja na fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 50.

Kupitia promosheni hii, wateja 10 wa Tigo wataweza kujishindia tiketi za kwenda kushuhudia mashindano haya makubwa barani Afrika, ambapo timu ya taifa, Taifa Stars nayo itakuwa inashiriki kwa mara ya kwanza baada ya miaka 36.

Ili wateja waweze kushiriki katika promosheni hii ya SOKA LA AFRIKA na kujipatia nafasi ya kuwa mamilionea pamoja na kushinda tiketi, watatakiwa kutuma neno SOKA kwenda 15670 au kutembelea tovuti ya www.tigosports.co.tzili kuweza kujibu maswali yanayoihusu mashindano hayo yanayofanyika nchini Misri.

SOKA LA AFRIKA ipo mahususi kwa ajili ya kuwazawadia wateja waaminifu wa Tigo ambao siku zote wamekuwa mstari wa mbele kutumia bidhaa na huduma za kampuni hiyo.

Fainali za Mataifa ya Afrika, ni mashindano makubwa kuliko yote barani Afrika ambayo yanawaleta pamoja wachezaji wa Kiafrika wanaoshiriki ligi kubwa na zenye ushindani ndani na nje ya bara la Afrika.

Zaidi ya wateja mia moja watashinda fedha kila siku, kila wiki na kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu nakadiri mteja anapojibu maswali, ndivyo anavyozidi kujiongezea pointi na nafasi kubwa zaidi ya kushinda tiketi kwenda Misri au mamilioni ya pesa.

No comments:

Post a Comment