Kampuni ya Tigo Tanzania, jana imetoa zawadi za mamilioni ya shilingi kwa mawakala wake wa huduma ya Tigo Pesa kupitia promosheni iliyomalizika hivi karibuni ya ‘Wakala Cash In Promotion’.
Promosheni hiyo ya nchi nzima ilianza Machi 1 na kumalizika Machi 31 ikilenga kuwahamasisha mawakala wa Tigo Pesa kufanya miamala zaidi na wateja ili kujishindia zawadi za fedha taslimu.
Akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa baadhi ya washindi jijijni Dar es Salaam jana,mkuu wa kitengo cha bidhaa wa Tigo Pesa James Sumari alisema jumla ya Mawakala 97,000 walishiriki katika promosheni hiyo ya mwezi mmoja.
“Promosheni hii ya aina yake, ni ya saba kwa Mawakala wetu. Tangu tulipoanza hadi kufikia hivi sasa, tumewazawadia mawakala 12,000 zaidi ya fedha taslimu shilingi bilioni 1. Washindi hawa wametoka kila kanda hapa nchini na tumeendelea kuona mwitikio mkubwa wa Mawakala kupitia promosheni hii na ni mpango wetu kuendelea kuwarushia tunachokipata kupitia wao wakati tukiendela na safari ya kufikisha huduma jumuifu za kifedha nchi nzima,” alisema Sumari
Kwa mujibu wa Sumari, Promosheni ya mwaka huu, ilishuhudia washindi wakubwa 8 kutoka sehemu mbali mbali za nchi ambao waliweza kujishindia fedha zaidi kutokana kuwa washindi wa jumla kwenye promosheni.
“Tumechagua Mawakala wawili waliofanya vizuri kuliko wengine katika kanda zote nne na kuwazawadia kutokana na jitihada zao za kufanya miamala mingi zaidi na wateja. Leo pia tunawashindi ambao watapata zawadi zaidi za fedha taslimu.
Washindi wakubwa ambao leo wanakabidhiwa zawadi zao wanatokea kanda ya Pwani ambao ni pamoja na Said Khatib kutoka Zanzibar ambaye atakabidhiwa shilingi milioni 2 na Mojelwa Mlinga Mojelwa kutoka Dar es Salaam ambaye amejinyakulia Shilingi milioni 1.
Tunayo furaha kuhitimisha promosheni yetu kwa kishindo.Tunaamini fedha tulizowazawadia Mawakala wetu zitawasaidia kukuza biashara zao pamoja na kukidhi mahitaji yao mengine. Napenda kumalizia kwa kumpongeza bwana Khatib na Mojewa pamoja na maelfu ya washindi wengine. Mchango wao unatusaidia kuweza kufikisha huduma jumuifu za kifedha hapa Tanzania kupitia Tigo Pesa,” alifafanua Sumari.
Sumari aliongeza kuwa, makabidhiano ya zawadi kwa washindi wa jumla katika kanda za Kaskazini, Kusini na Kanda ya Ziwa yatafanyika baadaye mwezi huu.
No comments:
Post a Comment